RONALDO BALAA AWEKA REKODI KALI ZAIDI KUWEKWA DUNIANI.
Mchezaji bora wa dunia Cristiano Ronaldo amezidi kuonyesha yeye ni bora duniani kwasasa baada ya jana kufunga magoli yote matatu wakati Real Madrid walipoifunga Celta Vigo kwa bao 3-0 mchezo wa ligi kuu Spain La Liga uliopigwa katika dimba la Santiago Bernabeu Jijini Madrid.
Magoli matatu aliyofunga jana yanamfanya Ronaldo kujiwekea Rekodi mpya ya kufunga magoli matatu au zaidi (Hat Trick) mara nyingi zaidi ya mchezaji yoyote katika La liga na pengine duniani. Akifunga hivyo mara 23 na hii ni tangu mwaka 2009 alipotua La Liga akitokea Manchester United
Ronaldo pia amefikisha idadi ya magoli 200 katika mechi 178 akiweka pia rekodi ya mchezaji aliyefunga magoli mengi zaidi kwa muda mfupi.
Alifunga goli la kwanza kwa njia ya penati dakika ya 36 ya mchezo kabla hajamalizia hat trick yake kwa magoli mawili kipindi cha pili yani dakika ya 65 na dakika ya 81 kabla hajatoka na nafasi yake kuchukuliwa na Javier Hernandez "Chicharito"
Real Madrid licha ya ushindi huo ilipata pigo baada ya mshambuliaji wake James Rodriguez kutolewa dakika ya 53 baada ya kuumia katika mchezo huo ambao Real Madrid waliweza kupiga mashuti 11 yaliyolenga goli huku Celta Vigo hawakuweza kupiga shuti lolote langoni mwa Real Madrid.
Magoli matatu aliyofunga Ronaldo jana pia yanamfanya afikishe magoli 23 katika mechi 14 tu alizocheza msimu huu katika La Liga.
Real Madrid kwa ushindi wa jana sio tu wameimarika kileleni mwa msimamo wa La liga lakini pia wamefikia rekodi iliyowekwa na Barcelona msimu wa mwaka 2005-2006 chini ya Frank Rijkaard kwa kucheza michezo 18 mfululizo bila kupoteza mchezo wowote na kama watashinda mchezo wao wa Jumanne wa ligi ya mabingwa Ulaya wataweza kuweka rekodi ya kuwa klabu ya kwanza toka La Liga kushinda michezo yote iliyocheza katika mashindano yote.
REKODI ZA HAT TRICKS NYINGI
- Cristiano Ronaldo - 23
- Alfredo Di Stefano - 22
- Telmo Zarra - 22
- Lionel Messi - 20
WACHEZAJI WALIOFUNGA MAGOLI MENGI PAMOJA NA IDADI YA MECHI - LA LIGA
- Lionel Messi (2004-mpaka sasa) - 253
- Telmo Zarra (1940-1955) - 251
- Hugo Sanchez (1981-1994) - 234
- Raul (1994-2010) - 228
- Alfredo di Stefano (1953-1966) - 227
- Cesar Rodriguez (1939-1955) - 223
- Quini (1970-1987) - 219
- Pahino (1943-1956) - 210
- Cristiano Ronaldo (2009-mpaka sasa) - 200
- Edmundo Suarez (1939-1950) - 195
.... Na Edo Daniel Chibo (0715 12 7272)
No comments