MAN UNITED vs STOKE CITY ~  STOKE ITAWEZA KUIZUIA TRENI ILIYOSHIKA KASI?



Kipute cha ligi kuu ya uingereza kinataraji kuendelea leo katika viwanja mbalimbali... Moja kati ya viwanja hivyo ni Ngome Kongwe ya Old Trafford nyumbani kwa Mabingwa wa historia wa ligi kuu England Manchester United ambao watawakaribisha Stoke City.



Man United ni kama Treni ambayo imeanza kuchanganya hivi sasa inatakiwa nguvu za ziada kuisimamisha na hii ni baada ya kuendelea kuimarika kila kukicha huku majeruhi nao wakirudi kikosini na itahitaji pointi tatu kuliko kitu chochote siku ya leo ili iendeleze rekodi yake ya kushinda mechi za ligi mfululizo.

Stoke City ambayo inanolewa na kocha ambaye amewahi kucheza Old Trafford kwa mafanikio makubwa itaingia katika mchezo wa leo ikiwa  imeshapoteza mechi sita mpaka sasa na kwa hali ilivyo haitakuwa tayari kuendelea kukosa pointi na kuzidi kudidimia

Man united inakamata nafasi ya 4 katika msimamo wa ligi ikiwa imeshajikamatia pointi zake 22 katika michezo 13 wakati Stoke City wao wanakamata nafasi ya 12 wakiwa na pointi zao 15.

Kwa Upande wa Manchester United Majeruhi yamekua yakiwakabili mno na mpaka tunaangalia habari za mechi hii ya leo wachezaji kadhaa wa United bado ni majeruhi ambao ni pamoja na Angel di Maria, Luke shaw, Daley blind, Phill Jones, Rafael da Silva, John Evance na Jesse Lingard .

Kwa upande wa Stoke City wao majeruhi pia yamewasumbua mno msimu huu kwani nao wana listi ndefu ya majeruhi wamiwemo Sidwel
Victor Mosses, Whelan, Huth, Peter Odemwingie
na Teixeira

FACTS


  • Rekodi zinaonesha kuwa Stoke City wamepoteza mechi zote 11 za michuano yote ambayo wamecheza na Man United katika dimba la Old Trafford, huku Robin Van Persie akiwafunga stoke magoli 10 katika mechi 9 alizopambana na Stoke City.
  • Mara ya mwisho timu hizi kukutana ilikua mwezi February mwaka huu wakati United walipokubali kichapo cha bao 2-1 katika uwanja wa Britania ushindi ambao ulikua ni wa kwanza kwa Stoke dhidi ya Man United  tangu mwaka 1984.
  • Stoke City hawajawahi kushinda Old Trafford tangu mwaka 1976 waliposhinda bao 1-0.


Na Sylvaction: Member : Wapenda Soka (Kandanda)

No comments

Powered by Blogger.