LEICESTER CITY VS LIVERPOOL - HISTORIA INAWAPA LEICESTER USHINDI.



Burudani ya ligi kuu nchini England Imerudi tena katikati ya wiki na leo kuna michezo kibao inapigwa katika madimba tofauti na pengine Wapenda Soka leo macho yetu yataangazia mechi ambazo zitaangaliwa na mashabiki wengi sio tu Tanzania bali Duniani.



Baada ya kusuasua na matokeo Mabaya msimu huu hatimaye kocha Brendan Rodgers alichukua maamuzi magumu ya kumwacha benchi nahodha Steven Gerard katika mechi iliyopita ambayo Liverpool walishinda bao 1-0 goli la kujitoa muhanga kwa beki Glen Johnson.

Licha ya ushindi huo mwembamba Liverpool walionekana kuzidiwa mno na vijana wa Mark Hughes na hii ndiyo inayowapa presha mashabiki ambao wanaamini Liverpool hii bado sana kufikia kiwango cha Liverpool ya msimu uliopita.

Liverpool wataingia katika pambano la leo wakitegemea kupata matokeo mazuri wakichagizwa na ushindi wa mechi iliyopita japokua haitakua rahisi kwani uwanja wa King Power hautabiriki na hapo unaweza tu kujikumbusha siku ile Man United walipopigwa bao 5-3 na Leicester City licha ya kutangulia kufunga.

FACTS

Mara ya mwisho timu hizi kukutana ilikua mwaka 2004 ambapo zilitoka sare ya bila kufungana katika uwanja wa Leicester

Katika mechi 13 zilizopita baina ya timu hizo Liverpool wameshinda mara 4 wakati Leicester wameshinda mara 5 na mara 4 timu hizo zilimaliza kwa sare.

No comments

Powered by Blogger.