MAN UNITED YAENDELEZA DOZI LIGI KUU ENGLAND
Manchester United wameendeleza dozi ya vipigo kwa timu wanazokutana nazo baada ya kuwabamiza Stoke City bao 2-1 katika mchezo wa ligi kuu England uliopigwa usiku huu katika dimba la Old Trafford.
Maroane Fellaini akifunga goli la kwanza kwa kichwa dakika ya 21 tu ya mchezo baada ya kuunganisha krosi ya Ashley Young upande wa kushoto wa uwanja.
Nzonzi akaisawazishia Stoke City bao dakika ya 39 kufatia makosa ya mabeki wa Manchester United kushindwa kumzuia Bojan ambaye alionekana kuwasumbua mabeki hao.
Bao la ushindi la United lilipatikana dakika ya 59 kupitia kwa Juan Mata baada ya kupiga mpira wa adhabu ndogo ukimshinda kipa Gegovic na kujaa wavuni.
Kwa matokeo hayo Man united wanasogea kwa pointi katika nafasi hiyo hiyo ya 4 wakiwa na pointi 25 pointi moja nyuma ya Southampton wanaokamata nafasi ya 3. Stoke wao wako katika nafasi ya 13 wakiwa na pointi zao 15.
LIGI KUU ENGLAND - MATOKEO NA WAFUNGAJI WA MECHI ZA JANA
● Burnley 1-1 Newcastle
. George Boyd (34)
- Papiss Cisse (48)
● Leicester City 1-3 Liverpool
- Simon Mignolet OG (22)
- Adam Lallana (27)
- Steve Gerrard (54)
- Handerson (84)
● Man United 1-2 Stoke City
- Fellaini (21)
- Nzonzi (39)
- Mata (59)
● Swansea 2-0 QPR
- Ki (78)
- Routledge (83)
● Crystal Palace 0-1 Aston villa
- Benteke (32)
● West Brom 1-2 West Ham
- Dawson (10)
- Nolan (35)
- Tomkins (45)
... Tufollow katika instagram @wapendasoka
No comments