JUVENTUS YAPUNGUZWA KASI NA FIORENTINA


Mabingwa watetezi wa ligi kuu nchini Italia kibibi kizee cha Turin klabu ya Juventus imepunguzwa kasi na Fiorentina kwa kulazimishwa sare ya bila kwa bila katika mchezo wa ligi kuu ya Italia maarufu kama Serie A.



Juventus wanaoongoza Ligi hiyo walikua na nafasi nzuri ya kuwakimbia AS Roma walio katika nafasi ya pili kama wangeshinda mechi hiyo na hivi sasa licha ya kuendelea kuongoza lakini kuna uwezekano tofauti ya pointi kati yake na As Roma ikapungua na kubaki moja iwapo Roma watashinda katika mechi ya Jumamosi hii dhidi ya Sassuolo

Juan Quadrado na mkongwe Mario Gomez wa Fiorentina walionekana kuisumbua sana ngome ya Juventus lakini juhudi za hazikuzaa matunda wakati upande wa Juventus Paul Pogba,Fernando Loriente na Carlos Tevez hawakuweza kubadilisha matokeo.

Kwa matokeo hayo Fiorentina wamefikisha pointi pointi 20 katika nafasi ya 8 huku Juventus wakibaki kileleni wakiwa na pointi 35.

+++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++

No comments

Powered by Blogger.