BORUSSIA DORMUND KUKIMBIA BALAA LA KUSHUKA DARAJA USIKU HUU.



Klabu ya Borussia Dortmund ambayo misimu miwili iliyopita ilikua moto wa kuotea mbali leo hii itaingia katika uwanja wake wa nyumbani Signal Iduna Park kujaribu kujikwamua na balaa la kushuka daraja msimu huu.



Dortmund ambayo inakamata mkia katika msimamo wa ligi kuu nchini Ujerumani maarufu kama Bundesliga wataikaribisha timu ngumu ya Hoffenheim ambayo inakamata nafasi ya 7 katika msimamo wa ligi.

Ikiwa imeshinda mechi 3, ikitoa sare mara 2 na kufungwa michezo 8, Borussia Dortmund wamejikusanyia pointi 11 tu wakati Hoffeinheim wao wameshacheza michezo 13 kama Dortmund wakishinda mechi 5, wakitoa sare mara 5 na kufungwa mara 3 huku wakiwa wamejikusanyia pointi 20 katika nafsi ya 7.

Kama Dortmund ikishinda pambano hilo itapanda mpaka ya 14 na kurudisha matumaini ya kufanya vizuri msimu huu lakini kama itafungwa itamuwia ngumu sana kocha Jagen Klopp ambaye Wapenda Soka Duniani wamekua wakimwamini kama kocha bora kabisa katika medani ya soka.

Matts Hummels anaweza kurudi toka majeruhi ili kumsaidia beki wa kati Mathias Ginter,Sebastian Kehl na Ilkay Gundogan wanaweza kucheza nafsi ya Kiungo kwa Upande wa Dortmund.
Sokratis, Dong-Won Jina Marvo Reus wataikosa mechi hi kutokana na majeruhi

Jin-Sun Kim anaweza kuanza katika mchezo huo akiwa  kama beki wa pembeni wakati Antony Modeste au Sven Schipplock wataanza pale mbele kwa kwa upande wa Hoffenheim.
Hoffenheim pia watawakosa Koen Casteels na Adam Szalai kutokana na sababu mbali mbali.

~ Edo DC

No comments

Powered by Blogger.