DORTMUND YAZINDUKA USINGIZINI
Baada ya kupoteza mechi 8 msimu huu Borussia Dortmund jana walizinduka na kuichapa Hoffenheim bao 1-0 katika mchezo wa ligi kuu nchini Ujerumani Bundesliga katika uwanja wa Signal Induna Park jijini Dortmund.
Dortmund waliingia katika mchezo huo wakiwa katika nafasi ya mwisho katika msimamo wa ligi kuu Ujermani wakiwa na pointi 11 tu hivyo ushindi pekee ndiyo ulikua unahitajika kuikwamua timu hiyo iliyofanya vizuri miaka miwili iliyopita kwa Ulaya na Ujerumani.
Goli pekee la Dortmund lilipatikana dakika ya ... ya mchezo kupitia kwa kiungo wa kijerumani Ilkay Gondugan goli ambalo liliamsha furaha kwa mashabiki zaidi ya elfu 70 waliojaza uwanja huo.
Kwa matokeo hayo Dortmund wametoka katika nafasi ya mwisho na kupanda mpaka nafasi ya 14 ambayo wanaweza kukalia kwa muda tu kwani mechi za leo zinaweza kuleta matokeo yanayoweza kubadili kabisa msimamo na pengine kuwarudisha Walikotoka.
+++++++++++++++++++++++++++
No comments