CHELSEA,MAN CITY ZAUA LIGI KUU ENGLAND
Kikosi cha Chelsea jana kilionyesha kuwa kinataka kumaliza msimu huu bila kufungwa baada ya kuifunga timu ngumu ya Totenham Hotspurs kwa bao 3-0 katika mchezo wa ligi kuu England katika dimba la Chelsea darajani ikiendeleza rekodi yake ya kucheza michezo 14 bila kufungwa mpaka sasa.
Chelsea iliyo katika kiwango kizuri hivi sasa ilianza kupata goli la kwanza dakika ya 19 tu ya mchezo likifungwa na Eden Hazard akipokea pasi murua ya Didier Drogba na dakika tatu badae Mkongwe Didier Drogba aliandika bao la pili kwa Chelsea na mpaka mapumziko Chelsea ilikua mbele kwa bao 2-0.
Kipindi cha Pili Chelsea waliingia kumalizia kazi iliyofanyika kipindi cha kwanza kwa kuongeza bao la tatu dakika ya 73 kupitia kwa Loic Remy akitumia vyema pasi ya Cisar Azpilicueta baada ya mabeki wa Spurs kujichanganya.
Kwa matokeo hayo Chelsea wameendelea kukaa kileleni mwa msimamo wakiwa na pointi 36 wakati Spurs wao wana pointi zile zile 20 katika nafasi ya 10.
WAKATI HUO HUO
Mabingwa watetezi Manchester City waliibamiza Sunderland kwao bao 4-1 shujaa wa mchezo huo akiwa Sergio Kun Aguero aliyefunga mabao mawili peke yake moja akilifunga dakika ya 21 na lingine dakika ya 71.
Magoli mengine ya Man City yalifungwa na Stevan Joveyic na Pablo Zabaleta huku Sunderland ambao wikiend waliwabania Chelsea baada ya kutoka nao sare wakitangulia kupata bao dakika ya 19 kwa kazi nzuri ya Connor Wickham.
Matokeo hayo yameisogeza Man City kipoint kwa kufikisha pointi 30 ikiwa ni pointi 6 nyuma ya Chelsea wanaoongoza ligi hiyo wakati Sunderland wakibaki na pointi zao 14 katika nafasi ya 14.
+++++++++++++++++
No comments