CHELSEA VS SPURS DABI YA LONDON NZURI KUITAZAMA LEO
Ligi kuu ya Soka nchini England inaendelea leo usiku kwa mechi 3 kali kupigwa katika viwanja tofauti.
Mji wa London leo utakua bize na mechi mbili kali yani ile ya Arsenal wakiikaribisha Southampton na ile ya Chelsea na Totenham Hotspurs ambayo ni kwa lugha ya kisoka tunaiita London derby.
CHELSEA VS SPURS
Chelsea ikiwa inaongoza msimamo wa ligi kuu Hivi sasa itaingia katika mchezo wa leo lengo kuu likiwa ni kuendeleleza rekodi ya kutopoteza mchezo wowote msimu huu huku ikiwa na kumbukumbu isiyoridhisha ya sare ya bila kufungana na Sunderland.Upande wao Spurs watachagizwa na ushindi wa bao 2-1 walioupata katika mechi iliyopita dhidi ya Everton japokua wanakamata nafasi ya 9 ikiwa na pointi 20 sawa na Arsenal,Liverpool na Newcastle.
Diego Costa wa Chelsea ataikosa mechi ya leo baada ya kupata kadi 5 za njano na Kwa upande wa Spurs beki wao Kyle Naughton atakuwepo baada ya kutumikia mechi mbili nje huku Adebayor akiwa katika hatihati ya kucheza.
FACTS
Totenham haijawahi kushinda katika uwanja wa Stamford tangu mwaka 1990 wakitoka sare mara 8 na kupoteza mara 14.Mechi nne kati ya 6 zilizopita baina ya timu hizo ziliisha kwa sare.
Chelsea haijapoteza mchezo wowote katika mashindano yote wakishinda mara 15 na kutoka sare maraa 5.
MECHI ZINGINE LEO
10:45 PM. Arsenal vs Southampton
10:45 PM. Chelsea vs SPURS
10:45. PM. Everton vs Hull
10:45. PM. Sunderland vs Man City
No comments