ARSENAL YAFUKUZA MWIZI KIMYA KIMYA 



Arsenal jana iliendeleza staili yake ya kumkimbiza mwizi bila kupigs kelele ilipoibamiza timu ngumu ya Southampton kwa bao 1-0 kama walivyofanya wiki iliyopita walipoifunga West Brom bao 1-0.



Alikua yule yule shujaa wa msimu huu wa Arsenal Alexis Sanchez aliyefunga bao pekee dakika ya 89 katika mchezo huo uliopigwa katika dimba la Emirates

Southampton ni kama wamesimamishwa hivi sasa kuwapisha wakubwa wapite kwani mechi ya pili mfululizo wanapoteza ya kwanza ikiwa ni ile ya wikiendi iliyoisha kwa kubamizwa na Man City na mbaya zaidi mechi ijayo watakutana na Manchester United ambayo nayo imefanya kinyume cha Southampton kwa kushinda mchezo wa 4 mfululizo katika ligi.

Kwa matokeo hayo licha ya kufungwa Southampton bado wanakamata nafasi ya 3 na Arsenal wanakamata nafasi ya 5 huku Southampton wakiwa na pointi 26 wakati Arsenal wana pointi 23.

WAKATI HUO HUO


Hali imeendelea kuwa tete kwa kocha wa Everton Roberto Martinez baada ya jana kulazimishwa sare nyumbani ya bao 1-1 na Hull City.

Everton iliingia katika mchezo wa jana ikiwa na matumaini ya kuibuka na ushindi baada ya matokeo ya kupoteza kwa bao 2-1 ugenini wakifungwa na Totenham.

Goli la Everton lilifungwa na Lukaku kabla ya Aluko hajaisawazishia Hull City.
Kwa matokeo hayo Everton wanabaki na pointi 18 katika nafasi ya 11 wakati Hull wana pointi 12 katika nafasi ya 17.

No comments

Powered by Blogger.