SERGIO AGUERO NI SHIDAAH AIPIGA BAYERN MUNICH 3 PEKE YAKE.
"Wangekua katika nafasi gani Manchester City Msimu huu bila kuwa na Aguero?" Ni swali alilouliza mtangazaji John Champion wakati mshambuliaji wa Manchester City Sergio Aguero akifunga bao la pili kwa mabingwa hao watetezi wa ligi kuu England wakiifunga Bayern Munich katika ligi ya mabingwa barani Ulaya.
Sergio Aguero alifunga magoli matatu wakati timu yake ikiibuka na ushindi wa bao 3-2 dhidi ya mabingwa hao wa Ujerumani.
Aguero akifunga bao la kwanza kwa njia ya penati baada ya Beki wa Bayern Benatia kumwangusha alipokua akienda kufunga huku goli la pili akifunga dakika ya 85 kabla ya kufunga la ushindi dakika za nyongeza kabla ya mpira kuisha.
Bayern Munich walipata magoli yao kupitia kwa Xabi Alonso kwa njia ya adhabu ndogo na lile la pili likifungwa na Robert Lewandowski kwa kichwa.
Kwa matokeo hayo matumaini ya Man City yamefufuliwa kwani wamefikisha pointi 5 sawa na Roma na CSKA Moscow na mechi ya mwisho City watasafiri kuwakabili AS Roma wakati FC Bayern Munich watakua nyumbani kuwakabili CSKA Moscow.
++++++++++++++++++++++++++++++

No comments