MESSI APIGA HAT TRICK NA KUWEKA REKODI MPYA LIGI YA MABINGWA ULAYA
Wiki hii inaweza kuwa muhimu sana kwa Lionel Messi kwani baada ya wikiend kuvunja na kuweka rekodi mpya ya kupachika mabao katika La Liga usiku wa jana kaweka nyingine katika ligi ya mabingwa barani Ulaya.
Wakicheza dhidi ya Apoel Nicosia Barcelona waliweza kuibamiza timu hiyo ya Cyprus bao 4-0 huku Lionel Messi akifunga mabao matatu peke yake katika mchezo huo ambao Bayern Munich walihitaji matokeo ya ishindi.
Magoli matatu ya Messi usiku wa jana yalimfanya afikishe magoli 74 katika ligi ya mabingwa Ulaya akiwa na umri wa miaka 27 tu hivi sasa. Akiwa amevunja rekodi ya muda mrefu iliyowekwa na Raul ya kufunga magoli 71.
Messi sasa amemwacha mpinzani wake mkubwa Cristiano Ronaldo kwa goli 4 zaidi katika michuano hiyo ambayo Ronaldo ameshafunga magoli 70 mpaka sasa.
REKODI YA WAFUNGAJI BORA LIGI YA MABINGWA ULAYA
Lionel Messi (Barcelona) - Magoli 74Raul (Real Madrid, Schalke) - 71
Cristiano Ronaldo (Manchester United,
Real Madrid) - 70
Ruud van Nistelrooy (PSV Eindhoven,
Manchester United, Real Madrid) - 56
Thierry Henry (Monaco, Arsenal,
Barcelona) - 50
+++++++++++++++++++++++++

No comments