LIGI YA MABINGWA ULAYA : TUSIPOFUZU 16 BORA TUFUKUZWE - NASRI
Kiungo wa Klabu ya Manchester City ya England Samir Nasri amesema haoni haja ya wao kuendelea kuwepo katika kikosi cha Manchester City msimu ujao kama watashindwa kuvuka hatua hii ya makundi ya ligi ya Mabingwa barani Ulaya ambapo leo ana mchezo muhimu kwao watakapoikaribisha Bayern Munich katika dimba la Etihadi jjini Manchester.
Man City wanakamata nafasi ya nafasi ya mwisho katika kundi E wakiwa na pointi 2 tu baada ya kucheza michezo minne kundi ambalo linaongozwa na Bayern Munich wenye pointi 12 wakifatiwa na AS Romavwenye pointi 4 sawa na CSKA Moscow ambazo leo zitakutana katika mchezo wa mapema kabisa huko Moscow.
Kama Man City watashindwa kuifunga Bayern Munich itakua ndiyo mwisho wao katika michuano ya mwaka huu na Samir Nasri anaamini kuwa kwa fedha ambazo wamiliki wamewekeza haiji akilini kama watashindwa kuvuka hatua hii.
"Tunahitaji kufanya kitu lasivyo tutashuhudia wachezaji wapya wakichukua nafasi zetu" alisema Nasri mwenye miaka 27.
Manchester City hawajawahi kuvuka hatua ya 16 bora ambayo msimu uliopita walifika hatua hiyo na kama watatolewa itakua ni mara ya 3 katika miaka minne
"Tuwe wawazi ukiangalia mshahara wa kila mchezaji na viwango vya wachezaji wenyewe 90% ni wachezaji wenye hadhi ya dunia halafu tusivuke hatua hii ya ligi ya mabingwa Ulaya itakua si jambo jema" Alisema Nasri
Wamiliki wa Manchester City, Sheikh Mansour bin Zayed al-Nahyan na familia ya kifalme ya Abu Dhabi wameshatumia paundi milioni 750 wakinunua wachezaji tangu mwaka 2008.
REKODI ZA MANCHESTER CITY
- 2013-14: Hatua ya 16 Bora - wakitolewa na Barcelona
- 2012-13: Hatua ya Makundi
- 2011-12: Europa League hatua ya 16 bora (wakimaliza katika nafasi ya 3 katika Ligi ya Mabingwa Ulaya)
- 2010-11: Europa League hatua ya 16 bora
- 2009-10: Hawakushiriki
- 2008-09: Uefa Cup Robo Fainali
MECHI ZA LEO LIGI YA MABINGWA ULAYA
KUNDI E
20:00 CSKA Moscow vs AS Roma
22:45. Man City vs Bayern Munich
KUNDI F
22:45. APOEL vs Barcelona
22:45. PSG vs Ajax
KUNDI G
22:45. Schalke 04 vs Chelsea
22:45. Sporting Lisbon vs Maribor
KUNDI H
20:00. BATE vs Fc Porto
22:45. Shaktar vs Athletic Bilbao
..... kumbuka ku like page yetu katika facebook www.facebook.com/wapendasoka-Kandanda

No comments