LIGI YA MABINGWA ULAYA : CHELSEA YAMFUNDISHA DI MATEO MPIRA



Roberto Di Mateo Kocha aliyeipa Chelsea ubingwa wa Ligi ya Mabingwa barani Ulaya mara ya kwanza katika historia yake usiku wa jana alifundishwa soka na klabu yake hiyo ya zamani baada ya kukubali kichapo cha bao 5-0 akiwa na Schalke 04 ya Ujerumani ambayo anaifundisha hivi sasa.



Chelsea wakiwa ugenini waliweza kupata magoli yao kupitia kwa John Terry dakika ya pili tu ya mchezo kabla ya Willian hajafunga goli la Pili dakika ya 26 huku beki wa Schalke Jan Kirchoff dakika moja tu kabla ya mapumziko na kufanya Chelsea kuongoza kwa bao 3-0 mpaka mapumziko.

Kipindi cha pili kiliongeza neema kwa Chelsea baada ya kupata magoli mawili zaidi kupitia kwa mkongwe Didier Drogba na Ramires na mpaka mcheo unamalizika Chelsea 5-0.

MATOKEO NA WAFUNGAJI

● CSKA Moscow 1-1 AS Roma
Francesco Totti (43')
Vasily Berezutskiy (90')

● BATE Borisov 0-3 FC Porto
Héctor Herrera (56')
Jackson Martínez (65')
Cristian Tello (89')

● Manchester City 3-2 Bayern Munich
Sergio Agüero (21') (Pen)
Xabi Alonso (40')
Robert Lewandowski (45')
Sergio Agüero (85')
Sergio Agüero (90')

● Apoel Nicosia 0-4 Barcelona
Luis Suárez (27')
Lionel Messi (38')
Lionel Messi (58')
Lionel Messi (87')

● Paris Saint-Germain 3-1 Ajax Amsterdam
Edinson Cavani (33')
Davy Klaassen (67')
Zlatan Ibrahimovic (78')
Edinson Cavani (83')

● Schalke 04 0-5 Chelsea
John Terry (2')
Willian (29')
Jan Kirchhoff (44') (Own Goal)
Didier Drogba (76')
Ramires (78')

● Sporting Lisbon 3-1 NK Maribor
Carlos Mané (10')
Nani (35')
Jefferson (42') (Own Goal)
Islam Slimani (65')

● Shakhtar Donetsk 0-1 Athletic Bilbao
Mikel San Jose (68')

No comments

Powered by Blogger.