NEWCASTLE NOMA YAIKIMBIZA MAN UNITED KIMYA KIMYA.



Licha ya kuanza ligi kwa kusuasua Newcastle imeamka na kushinda mchezo wake wa 4 mfululizo katika mwendelezo wa Ligi kuu Nchini England baada ya kushinda bao 2-0 ugenini wakiifunga West Bom.



Kocha Allan Pawdew ambaye wengi wetu tulijua angefukuzwa baada ya matokeo mabaya katika mechi 3 za mwanzo amedhihirisha kuwa alihitaji muda baada ya kuiwezesha timu hiyo kupanda mpaka nafasi ya 7 wakiwa na pointi 16 sawa na Manchester United wanaokamata nafasi ya 6.
 

Goli la kwanza la Newcastle na lilifungwa na Ayoze akiunganisha pasi ya beki wa Pembeni Janmaat dakika ya 45. Fabricio Coloccini aliipatia Newcastle bao la pili dakika ya 62  kufuatia pasi nyingine murua ya beki Daryl Janmaat  ambaye alikua nyota wa mchezo wa leo.

Tazama goli la Ayoze hapa


MATOKEO MENGINE

Sunderland 1-1 Everton
Tottenham Hotspurs 1-2 Stoke City
Mchezo unaoendelea hivi sasa ni Swansea vs Arsenal

++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++

No comments

Powered by Blogger.