ARSENAL HOI YACHAPWA 2-1 NA SWANSEA 



Baada ya sare ya bao 3-3 katikati ya wiki katika ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Anderletch Klabu ya Arsenal leo imekubali kichapo cha bao 2-1 kutoka kwa Swansea City katika mwendelezo wa Ligi Kuu Nchini England.



Licha ya kutangulia kufunga bao dakika ya 63 kupitia kwa mshambuliaji Alexis Sanchez ambaye yuko katika form hivi sasa baada ya kuwika katika mechi kadhaa za Arsenal zilizopita akiunganisha pasi ya Danny Welbeck.

Swansea City walirekebisha makosa na kupata goli la kusawazisha kupitia kwa Gylfi Sigurdson dakika ya 75 kabla ya Bafetimbi Gomis dakika 3 baadae.

Kwa matokeo hayo Arsenal wamebaki na pointi zao 17 wakishushwa kwa nafasi moja na hivi sasa wanakamata nafasi ya 6 wakiwapisha Swansea City ambao wao wamepanda mpaka nafasi ya 5 hivi sasa wakiwa na pointi 18.

Angalia magoli ya mechi hiyo hapa

1 comment:

Powered by Blogger.