MABINGWA ATLETICO MADRID HALI MBAYA SPAIN

Real Sociedad 2-1 Atletico Madrid

Real Sociedad wakiwa na msimu mbaya kabisa wameweza kuibuka na ushindi wa pili msimu huu wakiwafunga Real Madrid mechi ya kwanza na jana wakipata ushindi mujarab wa bao 2-1 wakiwafunga mabingwa watetezi Atletico Madrid katika mwendelezo wa mechi za Ligi kuu nchini Spain (La Liga)



Atletico walitangulia kufunga kupitia kwa Mario Mandzukic dakika ya 10 tu ya mchezo kabla ya Carlos Vella kusawazisha dakika 5 baadae.

Mchezo huo uliotawaliwa na ubabe mwingi ulishuhudiwa wachezaji 8 wa Atletico Madrid wakipata kadi za njano huku beki Siqueira akipata kadi nyekundu baada ya kupata kadi mbili za njano.

Real Sociedad walipata bao la pili dakika ya 82 ya mchezo kwa goli safi kabisa la mshambuliaji Imanol Agirretxe akiunganisha pasi ya Joseba Zaldua.

Aliyekua kocha wa Manchester United David Moyes amehusishwa kwa kiasi kikubwa kuchukua nafasi ya kocha Asier Santana katika kikosi cha Real Sociedad na kama angefunhwa jana ingekua ndo tiketi yake ya kuondoka katika kikosi hicho.

Na Kwa matokeo hayo Sociedad wamefikisha pointi 9 wakitoka katika nafasi ya mwisho mpaka nafasi ya 15 huku Atletico Madrid wao wamebaki na pointi zao 23 katika nafasi ya 4 timu zote hizo zikiwa zimeshacheza mechi 11 katika ligi kuu nchini Spain inayoongozwa na Real Madrid wenye pointi 27 ikifuatiwa na Barcelona yenye pointi 25.

MATOKEO MENGINE

Sevilla 1-1 Levante
Espanyol 1-1 Villareal
Valencia 0-0 Atletico Bilbao.

No comments

Powered by Blogger.