LIGI KUU ITALIA - JUVENTUS YAIPIGA PARMA WIKI
Mabingwa watetezi wa Ligi kuu nchini Italia kibibi kizee cah Turin klabu ya Juventus imeivurumusha Parma mabao 7-0 yani sawa na siku za juma nzima.
Carlos Tevez, Fernando Lolliente na Alvaro Morata walifunga mabao mawili kila mmoja huku beki Stephan Litchsteiner akifunga bao moja na kuizamisha kabisa Parma iliyosafiri mpaka katika jiji la Turin kujaribu kuwafunga mabingwa hao watetesi na mwisho wa siku kuishia kufungwa bao 7-0.
Kwa matokeo hayo Juventus wameendelea kujiimarisha kileleni baada ya kufikisha pointi 28 ikiwa ni tofauti ya pointi 3 dhidi ya AS Roma wanaokamata nafasi ya pili ambao jana walishinda bao 3-0 dhidi ya Torino.
++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++

No comments