NATAKA KUWA FERGUSON WA MILAN - INZAGHI


Kocha wa AC Milan Filipo Inzaghi 'Pipo' amesema anataka kupata mafanikio kama aliyopata Sir. Alex Ferguson akiwa na Manchester United.



Inzaghi ambaye ameichezea AC Milan miaka 11 aliteuliwa kuwa kocha wa timu hiyo mwezi June mwaka huu akichukua nafasi ya Clarence Seedorf aliyetimuliwa kutokana na matokeo mabaya.

Ni miezi minne tu imepita tangu Inzaghi mwenye miaka 41 na ambaye alikua mkali wa kufumania nyavu apewe jukumu la kuinoa klabu hiyo lakini ameshaanza kujitabiria mambo makubwa ambayo yatamchukua muda mrefu kuyakamilisha akitaka kufata mfano wa Si Alex Ferguson ambaye ameifundisha Man United kwa miaka 27 kabla hajastafua mwezi May mwaka 2013.

Rais wa klabu alishawahi kumtamkia Inzaghi kuwa angependa awe kocha wa Milan kwa miongo miwili zaidi na hiyo kumpa nguvu Inzaghi kujiamini.

Inzaghi anaamini pia washambuliaji wake Fernando Torres na Giampaolo Pazzini wataanza kufunga muda si mrefu baada ya Torres kufunga goli moja tu tangu amehamia Milan kwa mkopo akitokea Chelsea.

×××××××××××××××××××××××××××××××××××××××××××××××××××××××××××

No comments

Powered by Blogger.