MAJANGA MAN UNITED - DAVID DE GEA NJE MWEZI MZIMA
Majanga yanazidi kuikumba nafasi ya Ulinzi ya Manchester United baada ya kipa wake namba moja David De Gea kuteguka kidole katika mazoezi akiwa na timu yake ya taifa ya Spain.
De Gea mwenye miaka 24 na ambaye amecheza mechi zote 11 za ligi msimu huu akiwa na Manchester United huku akifanikiwa kutofungwa (clean sheet) katika mechi tatu yuko katika kambi ya timu ya Taifa ya Spain inayojiandaa kwa pambano la kirafiki dhidi ya Belarus.
Hii inakua habari mbaya sana kwa De Gea mwenyewe kwani alishaonyesha mwangaza wa kuwa kipa namba moja wa Spain akichukua nafasi ya Iker Casilas ambaye dhama zake zinakaribia kuisha.
Pia ni habari mbaya kwa kocha wa Man United Luis Van Gaal kwani sasa itabidi aamue kumtumia Anders Lindegaard ambaye alishaambiwa kuwa anaweza kuondoka United au pengine akamtumia kipa chipukizi Ben Amos.
Wiki hii pia tumeshuhudia Michael Carick akiumia na kuongeza list ya majeruhi kataka klabu ya Manchester United wakiungana na Marcos Rojo,Radamel Falcao,John Evans na Phil Jones.
De Gea atakaa nje mwezi mzima na atakosa mechi ijayo ya klabu yake dhidi ya Arsenal na atakosa mechi kati ya Spain na Ujerumani wiki ijayo.
------++++++++++++++++++++

No comments