ROONEY NAREKODI ZA HESHIMA LEO WEMBLEY
Ni usiku wa Wayne Rooney leo atakapokua akicheza mchezo wake wa 100 akiwa na timu ya Taifa ya England watakapoialika Slovenia katika mchezo wa kutafuta nafasi ya kucheza fainali za mataifa ya Ulaya ikiwa ni miaka 11 tangu alipocheza mechi ya kwanza mwaka 2003 akiwa na miaka 17 tu.
Rooney anaingia katika mchezo wa leo akiwa ameshacheza michezo 99 na kukamilisha historia ya kuwa kati ya wachezaji wanane tu katika historia ya timu ya soka ya England kufikisha idadi ya mechi hizo.
Historia inamweka Wayne Rooney katika nafasi ya 9 kati ya wachezaji ambao wameweza kufikisha mechi 100 wakiwa na timu ya taifa huku akiwa ndiye mchezaji pekee katika orodha ya wachezaji hao ambaye bado anaichezea England hivi sasa akiwa ameshacheza mechi 99 kabla ya mchezo wa leo.
××××××××××××××××××××××××
Orodha kamili iko hivi:-
- Peter Shilton [Golikipa] amecheza Mechi 125
- David Beckham - 115
- Steven Gerrard - 114
- Bobby Moore 108
- Ashley Cole - 107
- Frank Lampard - 106
- Bobby Charlton - 106
- Billy Wright - 105
- Wayne Rooney - 99
- Bryan Robson -90
Kwakufikisha mechi 100 Rooney atakabidhiwa kofia maalumu ya dhahabu ambayo ni heshima kwa wachezaji wote wanaofikisha mechi 100 kwa timu ya Taifa ya England maarufu kama Simba watatu.
Leo pi unaweza ukawa usiku wa kukumbukwa kwa nahodha Wayne Rooney kwa upande wa kupachika mabao kwani Rooney pia kama atafunga bao lolote leo ataweka rekodi ya kufikisha mabao 44 katika timu ya taifa ambayo inashikiliwa na mkongwe Jimmy Greaves ambaye katika mechi 57 tu alishafunga mabao 44.
Wakali wa mabao timu ya taifa ya England
- Sir Bobby Charlton: Amefunga Goli 49 katika Mechi 106
- Gary Lineker - Amefunga goli 48 katika mechi 80
- Jimmy Greaves - Amefunga magoli 44 katika mechi 57
- Wayne Rooney - Amefunga magoli 43 katika mechi 99
Mechi ya leo itaanza saa 2 kamili usiku kwa saa za Afrika Mashariki
+++++++++++++++++

No comments