RAIA WAWALAUMU DIEGO COSTA NA FABREGAS KUTOKUA WAZALENDO.
... Baada ya Kutojumuishwa kwa wachezaji Diego Costa na Cesc Fabregas katika kikosi cha timu ya Taifa ya Spain Raia wamewashutumu wachezaji hao kwa kutokua wazalendo.
Nahodha wa Spain Sergio Ramos amewataka Costa na Cesc kuwaondoa wasiwasi mashabiki wa spain kufatia uvumi huo.
Diego Costa na Cesc Fabregas licha ya kuichezea klabu yao ya Chelsea katika mchezo wake dhidi ya Liverpool watashindwa kuichezea Spain inayojiandaa na mechi mbili dhidi ya Ujerumani na Belarus hatua ambayo wengi wanaona kama wachezaji hao ni wasaliti na wanaithamini zaidi Chelsea kuliko Spain.
Costa na Fabregas ndo wachezaji wanaolipwa hela nyingi Chelsea kwa sasa na kutokuwepo kwao katika mechi za kimataifa itakua ni faraja kwa Kocha Jose Mourinho ambaye alipinga Spain kumtumia Costa ambaye ni majeruhi japokua yeye anamtumia.
~ Edo DC

No comments