MAOMBI YANAHITAJIKA KUINUSURU DORTMUND KUSHUKA DARAJA.
Ukiambiwa kuwa ile timu iliyocheza fainali ya Ligi ya mabingwa Ulaya pale Wembley Mwaka Juzi inashika nafasi ya mwisho unaweza usiamini lakini hali ndo hiyo kwa Borussia Dortmund kushika mkia katika ligi kuu ya Ujerumani baada ya kuchapwa bao 2-0 na Frankfurt.
Dortmund inapoteza mchezo wake wa 8 msimu huu katika michezo 13 iliyocheza na kwajinsi hali ilivyo kuna kila dalili za kocha aliyeonekana Bora duniani Jugen Klopp kufungashiwa virago baada ya matokeo hayo mabaya.
Ikisafiri mpaka jiji la Frankfurt kikosi cha Dortmund kilipata kipigo kingine ndani ya siku nne tu baada ya katikati ya wiki kuchapwa bao 2-0 na Arsenal katika michuano ya ligi ya mabingwa Ulaya.
Magoli ya Frankurt yalifungwa na Alexander Meir dakika ya 5 tu ya mchezo huku lile la pili likifungwa na Haris Seferovic dakika ya 78.
Dortmund inakamata nafasi ya mwisho katika msimamo wa ligi kuu Ujerumani ikiwa na pointi 11 tu baada ya kucheza mechi 13 ikishinda mara 3 na kutoa sare mara 2.
"Ni Maombi tu yanayoweza kuitoa Dortmund hapo ilipo" hiyo ilikua comment ya mdau mmoja wa kundi la Wapenda Soka katika mtandao wa Whatsapp.
+++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
No comments