SOUTHAMPTON NGUVU YA SODA? YAONJA JOTO YA JIWE KWA MAN CITY
Zile mbio ndefu za timu ya Southampton zimepunguzwa kasi na Mabingwa watetezi Manchester City baada ya kukubali kichapo cha bao 3-0.
Ratiba ya mechi za Southampton inaonyesha kuwa ngumu kuanzia mechi hii ya leo kwani Jumatano atakutana na Arsenal na Jumamosi watakua nyumbani kuwaalika Manchester United.
Man City walianza kupata goli la kwanza kupitia kwa Yaya Toure dakika ya 61, Kabla ya Frank Lampard kuongeza la pili na baadae Gael Clichy kufunga bao la tatu bao ambalo ni la kwanza kwake tangu ajiunge na Man City akicheza michezo zaidi ya 100 katika ligi.
Ushindi huo wa Manchester City umeipandisha mpaka nafasi ya pili baada ya kufikisha pointi 27 ikiiteremsha Southampton mpaka nafasi ya 3 wakibaki na pointi zao 26 huku Chelsea ikiongoza ligi kwakua na pointi 33.
Man City wanakutana na Sunderland Jumatano wakati Southampton watakua London kuikabili Arsenal.
No comments