YANGA YAUA SHINYANGA WAKATI JKT RUVU IKITIBUA REKODI YA AZAM 



Yanga SC wametoa kipigo cha cha bao 3-0 kwa timu ngeni katika ligi kuu Stand United pambano lililopigwa uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga jioni ya leo.

Yanga walianza kupata bao la kwanza kupitia kwa mshambuliaji wake Mbrazil Jaja kipindi cha kwanza kabla ya Jerry Tegete kuongeza mengine mawili kipindi cha pili kupitia kwa Jerrison Tegete akifunga magoli yote mawili.

+++++++++++++++++++++++++++++++++++++
AZAM 0-1 JKT RUVU 
+++++++++++++++++++++++++++++++++++++

Katika pambano lingine lililopigwa uwanja wa Chamazi Mabingwa watetezi Azam FC walikubali kichapo cha 1-0 hii ikifuta kabisa rekodi ya Azam ya kucheza michezo yote ya ligi msimu uliopita bila kufungwa mpaka mechi ya leo walikua hawajafungwa mchezo wowote wa ligi.

Kwa matokeo hayo Azam FC, Yanga na Mtibwa zote zina pointi 10 huku Mtibwa ikiwa na kiporo cha mechi dhidi ya Mbeya City itakayopigwa kesho mkoani Morogoro.

********************************************

No comments

Powered by Blogger.