WAZEE WA SARE SIMBA KAMA KAWA MBEYA



******************************
PRISONS 1-1 SIMBA SC
******************************
Mwendo wa sare umezidi kuendelea kwa Wekundu wa Msimbazi Simba baada ya kulazimishwa sare ya bao 1-1 na Prisons ya Mbeya katika mchezo uliopigwa katika dimba la Sokoine Jijini Mbeya.



Simba itabidi wajilaumu wenyewe baada ya kushindwa kabisa kulinda goli walilopata dakika ya 8 ya mchezo kupitia kwa Emmanuel Okwi na kuwaruhusu Prisons kusawazisha dakika ya 89 ya mchezo kupitia kwa Hamis Maigo.

Kwa matokeo hayo Simba sasa imefikisha pointi 5 baada ya kutoka sare katika michezo yake yote mitano
Lakini kitu cha kuvutia katika mchezo huo ni kumwona tena kipa chipukizi Peter Manyika JR ambaye leo pia alikaa golini kwa upande wa Simba akionyesha Umahiri mkubwa sana.

Simba wana kazi ngumu mbele yao kwani mechi inayofata watakua Morogoro kucheza na Mtibwa Sugar ambao msimu huu wameonekana wako vizuri mno.

+++++++++++++++++++++++++*++**

No comments

Powered by Blogger.