EL CLASICO : REAL MADRID YAIPIGA BARCELONA 3-1. RONALDO MMMMMMH
Barcelona wameonja machungu ya kufungwa msimu huu baada ya kukubali kichapo cha bao 3-1 toka kwa mahasimu wao Real Madrid katika mchezo wa Ligi kuu nchini Spain maarufu kama La Liga. Hii ni mechi ya kwanza kwa Barcelona kufungwa ikiwa ilishacheza mechi 8 bila kufungwa goli lolote.
Iliwachukua dakika 4 tu kwa Barcelona kupata bao kupitia kwa Neymar akimalizia pasi ya Luis Suarez na kuwaacha Real Madrid midomo wazi.
Baada ya hapo Real Madrid walishambulia kwa kasi kubwa kasi ambayo ilizaa kadi tatu za njano kwa Barcelona akiwemo Lionel Messi ambaye alipata kadi ya njano pia
Dakika ya 38 Ronaldo alifunga bao la kusawazisha kwa njia ya penati baada ya Mpira uliopigwa na Marcelo kuzuiwa kwa mkono na mlinzi wa Barcelona Gerard Pique na kuzaa penati Iliyofungwa kiufundi na Ronaldo.
Goli la pili la Real Madrid lilifungwa na Pepe kwa kichwa akiunganisha kona ya Toni Kroos huku Karim Benzema akifunga bao la 3 akiunganisha krosi ya James Rodrigous ambayo haikuokolewa na mabeki wa Barcelona.
Katika mchezo huo ambao macho ya Wapenda Soka Duniani yalikua kwa Messi na Ronaldo waliokua wakiwania kuweka rekodi binafsi.
Ronaldo kama angefunga magoli matatu au zaidi Angevunja rekodi ya mchezaji aliyefunga magoli matatu au zaidi mara nyingi zaidi lakini Ronaldo akaishia kufunga goli moja ambalo limemfanya kufikisha goli lake la 16 katika mechi 8 katika ligi na goli lake la 20 la msimu huu katika mashindano yote.
Messi yeye alikua akiwania rekodi ya kuwa mfungaji bora kabisa kuwahi kutokea La Liga iwapo angefunga magoli mawili au zaidi lakini hakufanikiwa kufunga bao lolote
Kwa matokeo haya Real Madrid wanazidi kuisogelea Barcelona baada ya kufikisha Pointi 21 ikiwa ni pointi moja nyuma ya Barcelona wanaoongoza ligi hiyo wakiwa na pointi 22 timu zote hizi zikiwa zimeshacheza mechi 9.
No comments