WENGER UWEZO UNAO,SABABU UNAYO,IMEBAKI KAZI MOJA TU YA KUMCHAPA ADUI YAKO
.
Historia inasema Mwaka 1971 nduli Idd Amin aliingia madarakani kama Rais wa Uganda, Alimkuta tayari Mwalimu Nyerere ameshakuwa Rais wa Tanzania. Licha ya kuwa Nyerere alimtangulia Iddi Amin kama Rais lakini Pia Nyerere alikua mkubwa kwa umri kuliko nduli Amin.
Lakini hiyo haikuwa sababu ya Nduli Amin kumuheshimu Mwl. Nyerere. Nduli Idd Amin hakumuheshimu Nyerere kwasababu alikuwa akiionea Tanzania na Nyerere vile atakavyo. Mwaka huo huo wakati anaingia madarakani alijaribu kuvamia Mji magharibi(Kagera),Ingawa hakufanikiwa lakini bado alifanikiwa kuitesa kidogo Tanzania.
Idd Amin bado akaendelea kumdharau Nyerere na Tanzania yake,Siku moja alimwandikia barua Mwalimu Katika barua hiyo Dada alimmwambia Nyerere hivi "Nataka nikuhakikishie kwamba nakupenda sana, na kama ungelikua mwanamke basi ningefikiria jinsi ya kukuoa japo kichwa chako kimejaa mvi. Lakini kwakuwa wewe ni mwanaume basi uwezekano huo haupo". Kwa Kashfa hii Nyerere hakujibu kitu. Bado Amin akaendelea kutembea kifua mbele huku akiamini Tanzania na Nyerere si kitu.
Mwaka 1978 Iddi Amin alivamia tena Mji magharibi(Kagera),na kufanikiwa kuuteka Mji,Amin akaendelea kutamba na kusema kuwa alitumia dakika 25 tu kuiteka Kagera.Amin aliendelea “ na hii bendera imeandikwa chama cha mupinduzi,lakini mimi nataka nyinyi siku ngine kama maneno itakuwa mbaya nyinyi mtarudi mtasafisha mpaka Dar-es-salaam”.Baada ya hayo Nyerere uvumilivu ukamshinda
“Tunayo kazi moja Watanzania, tunayo kazi moja tu, ni kumpiga.Uwezo tunao Sababu tunayo na Nia tunayo.”Hayo ni maneno ya Nyerere baada ya kushindwa kuvumilia maneno na mambo ya Amin anayowafanyia Watanzania.Nyerere akafanikiwa kuiongoza Tanzania kumpiga Amin,Tangu Kupigwa kwake na Nyerere Amin hakusikika tena anaizungumzia Tanzania wala Nyerere.Alimuheshimu Nyerere Baada tu ya Kumpiga.
Yaliyomkuta Nyerere kwa Amin ni kama kesi ya Wenger kwa Mourinho.Licha ya Wenger kumzidi Mourinho umri na muda wa kazi lakini Mourinho hamuheshimu Wenger hata kidogo. Mourinho anamdharau Wenger kwasababu kila siku akikutana naye anamfunga,Mpaka sasa ameshamfunga mechi 7 kati ya 12 walizokutana,Tangu Mourinho arejee nchini uingereza kikosi cha Arsene wenger akijafunga hata goli moja kwenye lango la Chelsea,Mechi 4 za mwisho Chelsea chini ya Mourinho imeshaifunga Arsena bao 10 huku Arsenal hawajafunga hata goli moja.
Unafikiri Mourinho ataanzaje kumuheshimu Wenger? Kama kila siku akikutana naye anampa kipigo cha uhakika kwanini asitembee kifua mbele dhidi ya Wenger?.Hata mimi ningekuwa Mourinho ningekuwa nina kila sababu ya kumuita Wenger ‘Specialist in Failure’
Wenger uwezo wa kufuta aibu anayoipata kutoka kwa Chelsea na morinho anao,Sababu ya kuwa juu ya Chelsea anayo ila anaonekana hana nia tu. Ukiangalia Chelsea na Arsenal utagundua ni klabu mbili tofauti. Kwa Uingereza ukiacha Manchester United hakuna timu nyingine yeyote inayoifikia Arsenal Kiutajiri. Arsenal ina uwezo mkubwa wa kutumia kuliko Chelsea,Lakini leo hii ukiangalia Kikosi cha Chelsea huwezi kufananisha na cha Arsenal hasilani. Chelsea wana kikosi kilichoshiba.
Arsenal kwa utajiri walionao ilibidi wawe na kikosi kizuri zaidi ya Chelsea,Lakini haipo hivyo. Hiyo yote ni kutokana na sera mbovu za usajiri za Arsene Wenger. Sera za Wenger ndio zinamponza kila siku kupigwa na kunyanyasika na timu zinazofanya usajiri mzuri kuliko yeye.
Wakati Mourinho ana Diego Costa wenger ana Danny Welbeck, Katikati Mourinho ana Nemanja Matic wakati Wenger ana Flamin. Hiyo ndio tofauti yao huo ndio ujinga unaomfanya Wenger aendelee kuwa ‘kubwa jinga’ kwa Mourinho.
Wenger hana ujanja zaidi ya kutumia pesa nyingi kuwaleta wakina khedira na Cavani kama kweli ana nia ya kuondokana na aibu anayopata kila siku kutoka kwa Mourinho.
Najua Wapenda Soka Wengi watapinga na kuniambia Wenger hana sababu ya kufanya usajili kwa ajili ya kumfunga Mourinho tu ila niwaambie tu hapa Mourinho nimemtolea mfano tu.
Maana yangu kubwa Ni kuwa Wenger lazima afanye usajiri wa Nguvu ili aweze kushindana na timu nyingine kubwa zenye kaliba ya Arsenal kama Bayern Munich, Man United, Real Madrid na Barcelona. Timu hizo nne ukijumlisha na Arsenal ndio timu 5 Tajiri Duniani lakini timu hizo nne ni tofauti kabisa na Arsenal ndani ya uwanja.
Wenger inabidi awe na nia ya dhati kama Nyerere ya kuondoka kwenye utumwa wa kuonewa na nduli Iddi Amin. Najua Uwezo anao,Sababu anayo ila hana budi kubadilishe nia yake kwa kuanza kutumia utajiri wa arsenal ipasavyo ili aende sawa na wapinzani wake. Wenger kama anataka heshima yake irudi ni lazima aanze tena kuwaadabisha wapinzani wake. Sir Alex Ferguson alikua akimuheshimu Wenger kwasababu alikua akimchapa. Ndani ya miaka 10 ya kwanza ya Arsene Wenger akiiongoza Arsenal alikua amemfunga mechi nyingi Fergi kuliko Fergi alivyomfunga yeye.Hiyo ilikua sababu tosha ya Fergi kumuheshimu. Lakini Mourinho hatamuheshimu Wenger mpaka pale atakapomchapa.
Na allen kaijage
0655106767
Kaijagejr@gmail.com

No comments