ARSENAL MAJANGA : OZIL NJE MPAKA MWAKA 2015
"Majanga juu ya majanga" ni kauli zilizoandikwa na wadau wengi wa Arsenal katika mitandao ya jamii. Frankinho na Chardboy toka Kundi la Wapenda Soka katika mtandao wa Whatsapp walikua ni kati ya wadau ambao walisikitika habari zilipotoka kuwa Kiungo mshambuliaji wa Arsenal Mesuit Ozil hataonekana tena uwanjani mpaka mwaka 2015.
Ozil atakua nje kwa muda wote huo kutokana na kuumia goti katika mechi ya wikiendi iliyopita dhidi ya Chelsea ambao Arsenal walikubali kichapo cha bao 2-0 ambapo Ozil alilazimika kucheza dakika zote 90 lakini badae akaenda kuripoti kwa madaktari wa Arsenal.
Badae alienda Ujerumani kujiunga na timu ya taifa lakini vipimo vilivyofanyika huko aligundulika kuwa ameumia goti na atakaa nje kwa wiki 10 mpaka 12.
Kinachowafanya mashabiki wa Arsenal kuona haya majanga ni kwakua Ozil anaongeza idadi ya wagonjwa ambapo ataungana na Olivier Giroud, Mathieu Debuchy, Aaron Ramsey, Theo Walcott, Serge Gnabry, Yaya Sanogo,Mikel Arteta na Abou Diaby ambaye bado hayuko vizuri sana licha ya kuanza kucheza.
×××××××××××××××××××××××××××××××××××××××××××××××××××××××××××

No comments