SIMBA NA SARE ZAKE MPAKA SAUZI
![]() |
Wachezaji wakitoka uwanjani |
Sare zimeendelea kutawala mtaa wa msimbazi katika klabu ya Simba baada ya leo tena kutoka sare ya bila kufungana na Timu ya Orlando Pirates inayoshiriki ligi kuu nchini Afrika Kusini katika mchezo mkali wa kirafiki uliopigwa katika uwanja wa Rand Asubuhi ya leo jijini Johannesburg Afrika Kusini.
Pambano hilo lilikua ni maandalizi ya mechi zinazofata kwa Simba katika ligi kuu Tanzania bara inayoendelea ambayo katika michezo yake yote mitatu Simba imetoka sare yote lakini pia ni mahusudi kwajili ya kujiandaa na pambano lake dhidi ya Yanga siku ya jumamosi ya tarehe 18 Mwezi huu.
Simba iliyoweka kambi yake ya mazoezi huko Sauzi iliingia katika mchezo wa leo ikiwakosa wachezaji wake walio katika timu za Taifa kama Miraji Adam, Kiemba, Okwi,Chanongo, Joram Mgeveke,Said Ndemla na Jonas Mkude.
×××××××××××××××××××××××××××××××××××××××××××
No comments