ARGENTINA YA MESSI,DI MARIA NA AGUERO HOI KWA BRAZIL.



Kikosi cha timu ya Taifa ya Argentina kilichosheheni nyota kibao wakiwemo Lionel Messi,Angel Di Maria,Pastore,Mascherano n.k wamekubali kichapo cha bao 2-0 toka kwa timu ya taifa ya Brazil.



Argentina ambao walionekana kucheza vyema katika pambano hilo lililopigwa katika dimba la "kiota cha ndege" jijini Beijing China walikubali kufungwa goli 1 kila kipindi.

Shujaa wa mchezo huo alikua mshambuliaji wa Atletico Mineiro Diego Tardelli aliyetupia magoli yote mawili la kwanza akifunga dakika ya 28 baada ya uzembe wa mabeki wa Argentina wakiongozwa na Mkongwe Pablo Zabaleta.
Goli la Pili alilifunga dakika ya 64 na kuzima kabisa ndoto za Argentina kuibuka na  ushindi katika pambano hilo ambalo Neymar na Messi ambao wanacheza pamoja katika klabu ya  Barcelona.

Katika mechi hiyo Lionel Messi alikosa penati iliyotolewa baada ya Angel Di Maria kuangushwa katika eneo la hatari.

×××××××××××××××××××××××××××××××××××××××

No comments

Powered by Blogger.