HABARI 8 KALI ZA SOKA LEO IJUMAA



NYUMBANI


1. Simba SC wanaendelea na kambi yake ya mazoezi nchini Afrika Kusini kujiandaa na mechi dhidi ya watani wa jadi Yanga itakayopigwa tarehe 18 jijini Dar. Kesho Jumamosi Simba Itacheza mechi ya kirafiki dhidi ya Orlando Pirates ikiwa ni mojawapo ya program za kocha Patrick Phiri.

2. Klabu ya Mbeya City imeendelea kusaka pesa baada ya kutengeneza bahasha zenye nembo yake na mdhamini mkuu kampuni ya Binslum ambapo bahasha hizo zitauzwa na kuongeza mapato ya klabu.
Ikumbukwe Mbeya City inaingiza pesa nyingi katika mauzo ya jezi zake kwa kuweza kusimamia vyema uuzwaji wa jezi hizo wanapata pia mapato toka kwa wadhamini walionao kampuni ya Binslum na Coca Cola bila kusahau mgao wa Azam media na Vodacom.



3.  Kiungo mshambuliaji raia wa Benin anayechezea West Brom Stephan Sessegnon atakua ni mmoja wa wachezaji watakaotua jijini Dar tayari kwa pambano la Jumapili la Kirafiki dhidi ya Taifa Stars.
Stars itacheza na Benin katika mechi ya kimataifa ya kirafiki katika dimba la Taifa jijini Dar.

4. Ligi daraja la kwanza Tanzania bara inataraji kuanza kutimua vumbi kesho Jumamosi katika miji ya Dar es Salaam,Songea,Mufindi,Arusha,Mbozi,Moshi, Mwanza na Geita.

5. Tiketi za mechi ya Watani wa jadi SIMBA vs YANGA zitaanza kuuzwa siku 6 kabla ya mchezo huo yani tarehe 13.


ULAYA

6. Kocha mstaafu wa Manchester United Sir Alex Ferguson amefunguka na kuongea mengi kuhusu mwenendo wa mabingwa hao wa Kihistoria wa England lakini kubwa zaidi likiwa ni kumsifia Kocha wa sasa Luis Van Gaal kwa kazi nzuri anayoendelea kuifanya klabuni hapo.
Ferguson anaamini kuwa alichokifanya Van Gaal kupunguza wachezaji waliokuwepo na kuongeza wengine 6 ni njia bora ya kujenga utawala wake.

7. Majanga juu ya majanga kwa Arsenal kwani imeripotiwa kuwa Mlinzi wake Laurent Koscielny ameumia kisigino akiwa katika mazoezi na timu yake ya Taifa ya Ufaransa ambayo inajiandaa na mapambano ya kirafiki.

8. Mjadala mkubwa umezuka kufuatia hatua ya Chama cha soka nchini England kufikiria kutaka kucheza baadhi ya mechi za Ligi kuu England nje ya nchi hiyo lakini hasa nchini Marekani. Wengi wa mashabiki wamekataa mpango huo kwa kusema kuwa utazinyima baadhi ya timu mechi za nyumbani.


.... Edo Dani

No comments

Powered by Blogger.