NDOA YA ARSENAL NA MAJERUHI
Tangu kuhamia kwenye uwanja mpya mwaka 2006, club ya arsenal imekua ikikumbwa na majeruhi yasiyokua na suluhisho.
Mashabiki wanajipa moyo kua, labda msimu ujao utakua tofauti, labda flani na flani wakicheza pamoja tutachukua ubingwa. Lakini miaka inavyozidi kwenda hakuna unafuu wowote, rekodi ya majeruhi inazidi kupanda mlima.
Mesut ozil ni mwathirika wa hivi karibuni, na kama kuna shabiki wa arsenal hatanyanyua nyusi au kukuna kichwa kwa hali inavyoendelea basi zidhani kama hana mapenzi ya dhati na timu yake.
Wengi wamekua wakitamani kuona walcot ana ozil wakicheza pamoja, hii ni kwa sababu ya spidi/kasi ya walcot na uwezo wa özil wa kuwachezesha/kuwang'arisha wachezaji wa aina iyo.
Lakini tangu Ozil amefika mwaka jana, amecheza na walcot mechi tano. Mechi ya kwanza dhidi ya sunderland september 2013, Ozil alimuekea 'through pass" 2 na kumfanya walcot kubaki na kipa mara mbili, lakini walcot kukosa zote, mechi ya mwisho desemba 2013, walcot akimtengenezea ozil bao la kusawazisha dhidi ya everton. Mpaka leo hii hakuna dalili ya Ozil na walcot kucheza pamoja tena mpaka mwaka 2015.
Hivi ulishawahi kujiuliza chanzo cha majeruhi ni nini katika klabu ya Arsenal?
...Je ni:-
* nyasi za emirates ni laini sana?
* aina ya mazoezi wanayofanya arsenal?
* wachezaji kuficha maumivu mpaka pale yanapokua sugu?
* Matumizi ya dawa mbali mbali za urembo na vipodozi ?(kama za kuotesha nywele ambazo zina side effects)
* Staili ya kimchezo ya arsenal?
* Au wachezaji wanachezeshwa sana bila mapumziko?
* Wachezaji wa arsenal ni lege lege??
* Au ni bahati mbaya tu arsenal ina gundu???
Me sijui, labda wewe unajua. Lakini hali inavyozidi kua mbaya, ninapata mashaka kidogo. Arsenal kama kampuni naamini nalo wanalifanyia kazi hili.
July 2014, walifanya usajili wa kocha maalum kwa ajili ya kuangalia au kusimamia physical condition za wachezaji. Mmarekani Shad Forsythe.
Kabla ya hapo alikua akifanya kazi hiyo na kikosi cha taifa cha Ujerumani tangu 2006, tena kwa mafanikio makubwa mpaka walipochukua kombe la dunia ivi majuzi.
Alivyoajiriwa kusema ukweli mashabiki wa arsenal walipata moyo, labda mkombozi amekuja. Mimi mwenyewe nilifikiri labda sasa hata Abou Diaby ataanza kucheza mda wote.
Lakini kinyume na matarajio, majeruhi yamezidi maradufu na hali hii inatia shaka. Mwandishi wa blog maarufu ya arsenal ya arseblog raia wa ireland Andrew Mangan anasema Mr.Shad Forsythe kwa sasa atakua anajihisi kama nahodha wa meli ya Titanic kwa muda ule ilivyokua inazama.
Inachekesha sana na mimi ni kati ya watu waliocheka sana nilivyosoma makala yake ya leo. Ni kweli baada ya mafanikio yote ujerumani, sasa amefika arsenal, kila mtu aliona yeye ndo mwokozi lakini hakika, balaa limezidi.
Sidhani kama anaweza kulaumiwa. Nafikiri majeruhi ni sehemu ya mchezo, zaidi kwenye zama hizi za kisasa, ambako wachezaji wanacheza kila baada ya siku tatu, na madawa na vyakula ni mengi kila namna.
Kila timu inaweza kua na wachezaji wawili watatu ambao ni wakurutu kwa majeruhi (prone to injury). Lakini kwa kikosi cha arsenal, 50% ya wachezaji wa arsenal ni wakurutu kwa majeruhi.
Abou Diaby
Tomas Rosicky
Yaya Sanogo
Kieran Gibbs
Jack Wilshere
Theo Walcott
Mikel Arteta
Aaron Ramsey
Nitaongelea wachache, nishaanza kuchoka kuandika kuhusu hawa majeruhi..
■ Abou Diaby
Sina haja ya kumuongelea sana nafikiri mnamjua vizuri. Me ni shabiki mkubwa sana wa uyu jamaa, nafikiri aina yake ya uchezaji ni wa Yaya Toure na Paul Pogba tu pekee.
Msimu huu mkataba wake unaisha, nafikiri ndo itakua mwisho wa maisha yake ya arsenal.
Hajawahi fikisha mechi 30 ndani ya msimu mmoja tangu amekuja arsenal mwaka 2006.
■ Kieran Gibbs
Namkumbali sana uyu kijana. Ana miaka 25. Akiwa fit, arsenal ina beki mzuri sana wa kiingereza. Asipokuepo na akiwepo uwanjani ni rahisi kuona pengo lake haraka sana.
Hajawahi cheza mechi 30 za premier league ndani ya msimu mmoja, tangu amezaliwa.
■ Theodor Walcot.
Alivyofika arsenal, alisumbuliwa sana na matatizo ya bega. Na alifanyiwa operesheni ya bega ambayo ilikua ikimweka nje mara nyingi.
January mwaka huu alipata jeraha linaloitwa "Anterior cruciate ligament" linahusiana na maeneo ya magoti.
Sifa mbaya ya jeraha hili ni kwamba unapolipata kurudia hali yako ya kawaida ni kazi sana, ronaldo de lima, ivan cordoba, michael owen, ole gunnar solskajer na wengineo waulize watakuambia shida ya jeraha hili.
Oh na emmanuel frimpong, atakwambia pia alipata jeraha hili mara mbili. Mpaka leo anakaribia kusahaulika.
■ Aaron Ramsey na Tomas Rosicky.
Ni kati ya wachezaji ambao hawawezi maliza msimu bila kusikia "alikaa nje wiki kadhaa". Muda wowote anaeza akaumia.
■ Mikel Arteta
Tangu akiwa everton, rekodi yake ya majeruhi sio nzuri. Ndani ya msimu mmoja, ataumia mara 2 mpaka mara 3. Na ni nahodha wa arsenal.
■ Jack Wilshere.
Huyu ndo huwa simwamini kabisaaaa. Nikiuonaga kalala uwanjani naanza kushika kichwa, tangu ankle yake ilivyoumia mwaka 2011, jack has never been the same.
Msimu huu anajitahidi, lakini bado. Akiguswa tu, hata kwenye benchi utamuona Arsene wenger anaanza kuhaha..na kukuna kichwa.
Majirani zetu Manchester united, hawachezi mbali na majeruhi saivi. Physcho room inaripoti Man united ikiongoza kwa majeruhi 9, ikifuatiwa arsenal yenye majeruhi 8.
Ni hayo tu kwa leo, yako mengi. Tuyabakishe kwa kesho.Tukutane kwa makala nyingine, hapa hapa Wapenda soka blog siku nyingine. Maisha ni zawadi, Enjoy.
Cheers!!!
{FRANKINHO : Member Wapenda Soka}
No comments