HABARI 8 KALI ZA SOKA LEO JUMAMOSI


                                       NYUMBANI


1. Timu ya Taifa ya Tanzania kesho itakua uwanja wa Taifa jijini Dar Es Salaam kuwakaribisha Benin katika mchezo wa kimataifa wa Kirafiki ambao macho ya Wapenda Soka yatakua kwa kiungo mshambuliaji wa Benin anayekipiga Wes Brom ya England Stephan Sessignon.

2. Simba leo ilitoka sare ya 0-0 na Orlando Pirates ya Afrika kusini katika mchezo wa kujipima nguvu uliopigwa katika dimba la Rand jijini Johanneaburg Afrika Kusini.(habari hii iko kwa kirefu katika blog hii)



3. Kikao cha kamati ya Utendaji ya shirikisho la Soka nchini TFF kilifanyika leo kujadili sakata la klabu kukatwa asilimia 5 ya mapoto ya wadhamini kwaajili ya maendeleo ya soka la vijana na kusikitishwa na taarifa za upotoshaji wa jambo hilo na kuamua kuwafungulia mashtaka katika kamati ya nidhamu wote waliohusika na upotoshaji akiwemo wakili Damas Ndumbaro.

4. Timu inayofundishwa na Kocha mwenye maneno mengi Jamhuri Kiwelu Julio Mwadui FC imeanza vibaya michuano ya ligi daraja la kwanza baada ya kuchapwa bao 1-0 na Toto Afrika katika mchezo uliopigwa katika dimba la CCM Kirumba jijini Mwanza.

                               AFRIKA NA ULAYA

5. Timu ya Taifa ya Nigeria ambao ni mabingwa wa Afrika wameangukia pua baada ya kuchapwa bao 1-0 dhidi ya Timu ya Sudan katika pambano lililopigwa jijini Khatom Sudan kuwania kufuzu kwa fainali za mataifa ya Afrika mwakani.

6.  Brazil imeichapa Argetina bao 2-0 katika pambano la Kirafiki la Kimataifa lililopigwa katika uwanja wa kiota cha ndege jijini Beijing China (soma kwa kirefu taarifa hii katika blog hii)

7. Pengine ikawa rahisi kwa Manchester United kumsajili Kiungo Mdachi Wesley Sneidjer kufatia kiungo huyo kukiri hadharani kama klabu yake ya Galatasaray haijamlipa mshahara mwezi wa tatu sasa.
United ilimwania Mara mbili kipindi cha nyuma na jaribio hilo lilishindikana lakini sasa limerahisishwa.

8. Chelsea wametenga paundi milion 48 kumnasa kiungo wa Liverpool na timu ya taifa ya England Raheem Sterling. Liverpool wanaendelea kujadiliana na Sterling ili kumsainisha mkataba mpya ambao utamfanya alipwe paundi 100,000 kwa wiki.


..Imeandaliwa na Edo Daniel Chibo
Nicheki kama una lolote kupitia

0715 127272(Whatsapp)
wapendasoka@gmail.com (email)
Edo Daniel Chibo (Facebook)
Wapenda Soka - Kandanda (page katika facebook)

No comments

Powered by Blogger.