KOMBE LA MATAIFA YA AFRIKA : MABINGWA NIGERIA HALI MBAYA
Hali ni mbaya kwa mabingwa watetesi wa Afrika timu ya Taifa ya Nigeria baada ya jana kufungwa bao 1-0 na Sudan katika mfululizo wa mechi za makundi za kutafuta nafasi ya kushiriki fainali za kombe la mataifa ya Afrika mwakani huko Moroko.
Katika mechi hiyo ya kundi A Nigeria iliruhusu bao dakika chache kabla ya mapumziko kufatia mpira wa krosi uliochongwa na kuunganishwa na Abdi Bakri dakika ya 42.
Hii ni mechi ya pili Nigeria inapoteza baada ya kufungwa katika mechi iliyopita dhidi ya Congo huku wakitoa sare katika mechi ya awali dhidi ya Afrika Kusini.
Matokeo ambayo yanaifanya Nigeria kubaki na pointi moja tu katika msimamo wa kundi hilo ambalo linaongozwa na Afrika Kusini yenye pointi 7 ambayo jana iliifunga Congo Brazaville bao 2-0 huku nafasi ya pili ikishikwa na Hao Congo wakiwa na pointi 6 na Sudan inapointi 3 katika nafasi ya 3.
Mechi inayofata itachezwa Jumatano ambapo Nigeria itakua nyumbani kutaka kulipiza kisasi dhidi ya Sudan huku Afrika Kusini ikiikaribisha Congo katika mechi za hatua ya pili ya makundi.
××××××××××××××××××××××××××××××××××××××××××××××
No comments