PHIRI APEWE MUDA WA KUJENGA SIMBA YA MSIMU UJAO.
“Kazi ya
pamoja(Teamwork) inaleta matokeo mazuri, lakini maono hayo huwa ndoto pale
kiongozi anapokuwa na malengo makubwa huku akiwa na timu isiyostahiki”.Najaribu
kumuelewa John C Maxwell, Mchungaji maarufu na miongoni mwa watunzi bora wa
vitabu Marekani. Siku zote matokeo bora
huletwa na timu bora. Na timu bora ni ile inayofanya kazi kwa pamoja(teamwork). Lakini
ili upate timu inayocheza kwa pamoja na kwa umoja lazima utengeneze kitu
kinachoitwa ‘Chemistry’(kemia)
Kwenye
soka tumekuwa tukitumia maneno kama
chemistry (kemia) huku wengi tukiwa hatujui maana yake. Nilishawai kutoa maana ya
chemistry wakati naizungumzia Manchester ya Van Gaal. Nilisema “kemia ni masomo ya atomi na mkusanyo wa
atomi kuwa molyekuli. Yaani hizo atomi ukizichanganya utapata kitu kizima
kinachoitwa molyekuli. ukichanganya hydrogen na oxygen unapata maji, ukichukua
sodium na chlorine unapata chumvi na ukitaka kupata chumvi na maji kwa pamoja
ni lazima uchanganye "acid" na "base" Mchezaji ndio atomi yenyewe na timu ndio
molyekuli. Kitendo cha kuwaunganisha wachezaji katika timu moja na wachezaji hao
kuungana katika mfumo husika ndio tunaita chemistry(kemia). Kocha anaposhindwa
kupata wachezaji husika kwenye mfumo husika hapo ndipo tunasema kashindwa
kutengeneza chemistry kwenye timu. Na kushindwa kupata ‘chemistry’ kwenye timu
ndiko kunakofanya timu isicheze kwa maelewano na hapo ndipo tunapokosa teamwork”.

Ukiacha
Safu ya ulinzi kwenye kiungo pia kuna tatizo hilo hilo la kukosa muunganiko au
maelewano kwa lugha nyepesi. Kwizera, Mkude na Kisiga ni miongoni wa viungo bora
kabisa kwenye ligi kuu Tanzania. Kama ni vipaji hakika Mungu amewapa, lakini
mpaka sasa hawa watu wameshindwa kucheza pamoja kama timu. Kwizera, Kisiga na
Mkude ndio mara yao ya kwanza kucheza kwa pamoja kwenye timu moja. Kwa haraka
utagundua vipaji hivi maridhawa vimekosa kitu kinachoitwa “Chemistry”.
Nikimuangalia Emmanuel Okwi uwanjani namkumbuka Michael Jordan, Michael
Jordan ambaye inasemekana ni mchezaji bora wa kikapu kuwai kutokea
ulimwenguni, Jordan kila timu anayoichezea macho yote walikua wakimuangalia
yeye. Jordan alikuwa akijitahidi kwa hali na mali timu ishinde lakini mara
nyingine timu anayoichezea inapata matokeo mabaya yanayopelekea kukosa
kombe. Jordan alikua akiumia sana na siku moja ilibidi avunje ukimya na akasema
maneno haya “Kipaji kinaweza kushinda mechi, lakini akili na kufanya kazi kwa
pamoja ndipo kunashinda kombe”. Ukiangalia jitihada anazofanya Okwi uwanjani ni
kama wamemsusia timu. Hapati ushirikiano unaohitajika kutoka kwa wachezaji
wenzake, mpaka sasa Simba imefunga magoli 4 hakuna hata goli moja
lisilomuhusisha Okwi. Lakini ukiangalia kwa jicho la tatu utagundua washambuliaji
wa simba wamekosa ‘combination’, hapo ndipo tunarudi kule kule kwenye
“Chemistry”
Kabla ya
msimu huu kuanza simba ilitema wachezaji zaidi ya 11,Wachezaji 11 ni wengi
sana,ni sawa na kikosi kamili uwanjani.Ukichukua maamuzi magumu ya kutema
wachezaji 11 kwenye timu kwa msimu mmoja maana yake unataka kujenga timu
upya. Simba wana wachezaji wengi wapya, pia wana kocha mpya, japo inawezekana lakini si rahisi kwao kupata kombe kwa
msimu huu huku wakiwa na kila kitu kipya, kipa na mabeki wageni,viungo na
washambuliaji wapya.
Simba
chini ya kocha Phiri inabidi wapewe muda wa kujenga timu imara ya misimu ijayo, kupata
“Chemistry” kwenye timu kunahitaji muda wa kutosha. Simba inabidi impe uhuru kocha
Phiri msimu mzima, huku wakimuhakikishia kibarua chake ili afanye kazi ya
kujenga timu bila presha yeyote.Wapenzi na wadau simba inabidi wakubali
kuupoteza msimu huu kwa ajili ya misimu bora ijayo. Simba kwa kikosi hichi
walichonacho kina wachezaji wengi sana wenye vipaji. Nafikiri baada ya msimu huu
Simba watakua wameshapata “chemistry”, nafikiri Phiri atakua ameshachanganya
atomi zake vizuri na kupata molekyuli imara. Nina imani Simba wakifanya hivi
watarudi tena kama timu ya kuogopwa Afrika mashariki na kati.
Na allen kaijage
kaijagejr@gmail.com
0655106767
Na allen kaijage
kaijagejr@gmail.com
0655106767
No comments