HABARI 8 KALI ZA SOKA JUMATANO


                              NYUMBANI


1. Simba SC leo imemaliza mechi zake za kujipima nguvu kwa kichapo cha bao 2-0 toka kwa Jomo Cosmos ya nchini Afrika Kusini. huu ni mchezo wa tatu tangu Simba ilipotua jiji Johanesburg ikitoa sare na Orlando Pirets na Bidvest Wits.

2. Yanga imeendelea na mazoezi yake Kunduchi jijini Dar kujiandaa na pambano lake dhidi ya watani wa jadi Simba huku walinzi wawili Canavaro na Yondani wa timu hiyo ambao walikua majeuhi wakianza mazoezi mepesi tayari kujiweka sawa na pambano hilo.



3. Ligi daraja la Kwanza Tanzania bara iliendelea tena leo kwa timu kadhaa kushuka dimbani. Friends Rangers iliibamiza Afrikan Lyon bao 1-0 katika mchezo uliopigwa uwanja wa Karume jijini.

                                   
                               AFRIKA NA ULAYA

4. Ivory Coast imeangukia pabaya leo baada ya kubamizwa bao 4-3 na timu ya taifa ya Congo DRC katika pambano lililopigwa huku Salomon Kalou akipiga mabao mawili ambayo hayakusaidia. Kundi hili D linaongozwa na Cameroon ambao wana pointi 10.

5. Matumaini ya timu za afrika Mashariki Mashariki kushiriki fainali zijazo za kombe la mataifa ya Afika baada ya leo kuchapwa bao 1-0 na Togo.
Uganda iko kundi G ambalo linao.gozwa na Ghana halafu Togo.

6. Klabu Bingwa ya Ulaya Real Madrid huenda itakutana na mmoja kati ya Cruz Azul,Al Hilal au WesterncWanders katika mechi ya ufunguzi ya klabu Bingwa ya Dunia mwezi Disemba nchini Moroko. Mabingwa hao wataingia moja kwa moja hatua ya nusu fainali.

7. Mlinzi wa Real Madrid Rafael Verane amefunguka na kusema alikaribia kusaini kuichezea Manchester United mwaka 2011 ila kilichomkatisha tamaa ilikua kununuliwa kwa Phil Jones katika kikosi cha United.

8. Luis Suarez ameshinda tuzo ya kiatu cha dhahabu baada ya kufunga magoli 31 akiwa na Liverpool msimu uliopita kiasi cha magoli ambacho kinalingana na kile cha Cristiano Ronaldo tuzo ambayo ilikabidhiwa kwa Suarez na Kocha aliyempeleka Suarez Liverpool si mwingine ni Kenny Daglish.

... ASANTENI
.......Usisahau ku like ukurasa wetu Facebook (Wapenda Soka- kandanda)

{Edo Daniel Chibo}

No comments

Powered by Blogger.