PAUNDI MILIONI 10 KUMPELEKA KHEDIRA MAN UNITED
Klabu ya Manchester United imeweka mezani paundi milioni 10 kwa ajili ya uhamisho wa mwezi Januari wa kiungo wa Real Madrid Sami Khedira, Wapenda Soka Imeipata hiyo.
Kikosi cha United ambacho kinahaha hivi sasa kumpata kiungo wa kucheza dimba la kati baada ya waliopo kushindwa kuonyesha wanahimili mikimiki imeamua kuhamishia "majeshi" kwa kiungo huyu Mjerumani ambaye amekosa kabisa nafasi ya kucheza katika kikosi cha Real Madrid baada ya kuona ndoto zao za kumsajili Kiungo wa Roma Kevin Strootman kuonekana kushindikana baada ya Roma kutoa taarifa ya kutomuuza Kiungo huyo baada ya dirisha kufunguliwa na kama atauzwa basi haitakua chini ya paundi milioni 30.
Na United hawako tayari kutoa kiasi hicho cha pesa kwa mchezaji ambaye hajacheza mechi yoyote Tangu mwezi Machi alipoumia.
Inasemekana kocha Van Gaal ameambiwa na kaimu mtendaji mkuu wa klabu Edward Woodward kuwa atafute mchezaji mbadala wa Strootman ambaye atapatikana kwa bei rahisi na Khedira ameonekana kupewa nafasi hiyo.
Khedira mwenye miaka 27 mkataba wake na Madrid utaisha mwakani na paundi milioni 10 zinaonekana zitakubaliwa na Madrid kwani wasipochukua mchezaji huyo ataondoka bure pindi mkataba ukiisha.
Ikumbukwe Khedira alikua katika hatua nzuri za kusaini mkataba na klabu ya Arsenal lakini swala la mshahara wake lilikwamisha swala ambalo kwa United halitakua shida kutokana na kuhitajika vilivyo mchezaji huyo.
Na Edo Daniel Chibo
...USISITE KU LIKE PAGE YETU KATIKA MTANDAO WA FACEBOOK/WAPENDA SOKA - KANDANDA.
No comments