LIVERPOOL WALINUNUA SURUALI NYINGI NA KUSAHAU KUWA HAWANA SHATI
"Hatukustahili chochote, safari imekua ndefu na tuendako hakujulikani"
Hii ni kauli iliyotolewa na Nahodha wa Liverpool wenyewe wanamwita 'Fantastic Captain' Steven Gerrard.
Kauli ambayo wengi wanaweza kuiona kama kauli rahisi lakini mimi kwa Mtazamo wangu naiona kama ina maana kubwa sana kwenye ulimwengu wa soka hasa ikiwa imesemwa na nahodha wa timu kubwa kama Liverpool.
Mlima walionao liverpool ni mrefu sana na wasipojitazama vizuri watarudi kwenye zama za kale zama zakuishi kwa matumaini huku dawa zikiwa ni adimu na ni majirani tu wanaweza kuzimudu.
Swala ni lile lile ni vipi wachezaji zaidi ya tisa wapya wanaweza kucheza na kuleta matokeo kwa muda mfupi na hapa ndipo unapogundua matumaini na dawa tunayotumia ni tofauti kabisa.
Sawa inawezekana kusema wapo katika kipindi cha mpito lakini hebu jaribu kujiuliza Liverpool wako katika mpito upi?. Ni nani anayekupa wewe uwe katika kipindi cha mpito wakati kila kukicha wachezaji wanakuja na kuondoka.
Sasa hivi ni muda tu wa kuimba nyimbo za akina kasheshe kwakua matumaini yanapotea kabisa na kuzimika kama mapigo ya moyo.
Kocha wa Liverpool Brendan Rogers kwa sasa anaweza kua na presha kubwa kila anapo angalia ratiba za mechi zinazofata kwa timu yake na hii pengine inatokana na jinsi gani mipango na utekelezaji vinavyo kinzana.
Wakati wa dirisha la usajili Liverpool walikua kama wameokota fuko la pesa ambalo kwao lilikua kama la mkulima wa kule kwetu Lushoto ambaye amevuna na ameamua kwenda mjini kufanya manunuzi ya mavazi na mbaya zaidi akakuta soko limekua kubwa na kujikuta amenunua suruali nyingi huku shati akilinunua moja tu halafu bila kuelewa hilo shati alilonunua ni moja na mitoko ni mingi.
Nimemwangalia golikipa wa liverpool Simon Mignolet huyu kwa bahati mbaya hivi sasa amekua ni zaidi ya Steven Gerard yani kila mechi yupo na kiwango chake kinatia shaka huku akipata tabu sana kushirikiana na safu yake ya ulinzi.
Liverpool kwa sasa haina ushindani wa ndani ya uwanja tofauti na ilivyokua mwaka jana amebaki Rahim Sterling peke yake ambae utamaduni wa ligi na mpira wa England ni kua unapofikia katika kiwango bora basi wewe ni komandoo wa kila vita. Nakumbuka Kuna siku Savage alisema “they play too much at their young age” ni kweli Rahim Sterling anacheza sana tatizo linaanza ni kua anamaumivu ya uchovu na jinsi mpangilio ulivyo wa michuano ambayo Liverpool wanashiriki basi tunaeza anza kosa utamu wa Rahim Sterling ambaye amekua akiwasumbua sana mabeki wa timu pinzani na hapa ndipo ule wimbo wa the sinking ship (meli kuzama) utaanza kuimbwa.
Usishangange kumuona simba juu ya mti pita tu nenda zako hapa najiuliza huko waliko jificha mashabiki wa Liverpool wanasemaje juu ya usajili wa Mario Balotteli lazima tu kuna wanaotikisa kichwa na kumlaumu tu Baloteli ila mi nadhani ni mchezaji mzuri tofauti ni sehemu aliyopo na hapa ndipo unaweza kuaamini kua mpira hauna adabu.
Beki Jose Enrique hana uwezo tena wakuhimili mikikimikiki hii na hapo ndipo wanapojichelewesha wenyewe na yale mavazi waliyo nunua na kusahau mengine muhimu.
Dhahabu ni nzuri lakini ni ghali Liverpool kama na wao wanahitaji kutembea kifua mbele basi hawana sababu ya kujificha na kununua chuma huku wakiamini siku kitakua dhahabu bali ni muda wakupigana kumbo kutafuta dhahabu kama wafanyavyo majirani waswahili wanasema ngumi zikikuzidi tumia hata meno.
Kwa muda huu uliobaki ni dhahiri kua kocha Brendan Rodgers atakua anasoma kitabu cha tafsiri ili kupata maana ya maneno haya mawili disjoint na dysfunctional na kuya tumia kutatua matatizo ya Liverpool.
Imeandaliwa na
Lucas_ tz (Lucas Kifyasi): member of Wapenda Soka
0764665151
No comments