NEYMAR BALAA APIGA BAO ZOTE 4 BRAZIL IKISHINDA 4-0
Ilikua ni shoo ya Neymar mchana huu baada ya kupiga bao 4 peke yake akiiongoza Brazil kama nahodha kuiangamiza Japan goli 4-0 katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki uliopigwa katika uwanja wa taifa wa Singapore.
Neymar aliyefikisha mabao 40 katika timu ya Taifa ya Brazil katika mchezo wake wa 58 alifunga mabao yake katika dakika za 18, 48, 77, 81 na kumfanya kocha wa mpya wa timu hiyo kutofungwa mchezo wowote na haijafungwa goli lolote mpaka sasa.
Neymar anakua mchezaji wa 5 kufunga magoli mengi katika timu ya taifa akitanguliwa na Pele,Ronaldo, Romario na Zico
WAFUNGAJI BORA WA TIMU YA TAIFA YA BRAZIL
● Pele (77)
● Ronaldo (62)
● Romario (55)
● Zico (48)
● Neymar (40)
● Bebeto (39)
×××××××××××××××××××××××××××××××××××××××××××××××××××××××
No comments