INIESTA ASHINDA TUZO YA MGUU WA DHAHABU AWAZIDI KETE WAKINA RONALDO NA ROONEY
![]() |
Iniesta akiwa ameshika Tuzo yake ya mguu wa dhahabu |
Andres Iniesta jana alishinda tuzo ya mguu wa dhahabu mwaka 2014 iliyotolewa huko Monaco nchini Ufaransa kwa kuwashinda nyota wengine wanaong'aa katika soka akiwemo mchezaji bora wa Dunia Cristiano Ronaldo.
![]() |
Iniesta akivua viatu ili kuacha alama za unyayo wake |
Waandishi wa Habari huchagua majina ya wachezaji 10 waliofanya vizuri katika mwaka na kuyapigia kura na huu ni mwaka wa kumi zikitolewa Tuzo hizo.
Andres Iniesta anakua mchezaji wa kwanza wa Barcelona na Spain kushinda tuzo hiyo alishindanishwa pia na Cristiano Ronaldo, Nahodha wa England Wayne Rooney, Andrea Pirlo, Thiago Silva, Thiery Henry, Frank Ribery, Yaya Toure, Manuel Neuer na Marta.
Iniesta aliambatana na mkewe Anna Ortiz katika tuzo hizo ambazo zimewahi kuchukuliwa na wachezaji nyota kama Ronaldinho, Zlatan Ibrahimovic,Ronaldinho, Ryan Giggs n.k
![]() |
Katika Pozi Iniesta akiwa na Mkewe Anna |
WASHINDI WA TUZO HIZO TANGU ZILIPOANZISHWA
- 2003 - Roberto Baggio (Brescia)
- 2004 - Pavel Nedved ( Juventus)
- 2005 - Andriy Shevchenko (AC Milan)
- 2006 - Ronaldo De Lima (Real Madrid)
- 2007 - Allesandro Del Piero (Juventus)
- 2008 - Roberto Carlos (Fanerbahce)
- 2009 - Ronaldinho (AC Milan)
- 2010 - Francesco Totti ( AS Roma)
- 2011 - Ryan Giggs (Manchester United)
- 2012 - Zlatan Ibrahimovich ( PSG)
- 2013 - Didier Drogba ( Galatasaray)
- 2014 - Andres Iniesta (Barcelona)
.... Imeandaliwa na Edo Daniel Chibo
++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
Hiii tuzo hata giggs ameshachukua sio mchezo
ReplyDelete