INIESTA ASHINDA TUZO YA MGUU WA DHAHABU AWAZIDI KETE WAKINA RONALDO NA ROONEY

Iniesta akiwa ameshika Tuzo yake ya mguu wa dhahabu

Andres Iniesta jana alishinda tuzo ya mguu wa dhahabu mwaka 2014 iliyotolewa huko Monaco nchini Ufaransa kwa kuwashinda nyota wengine wanaong'aa katika soka akiwemo mchezaji bora wa Dunia Cristiano Ronaldo.

Iniesta akivua viatu ili kuacha alama za unyayo wake
Tuzo hiyo ya kimataifa inayotolewa kwa mchezaji aliyefanya vizuri yeye kama yeye na yeye akiwa na timu na hutolewa na wachezaji walio na umri wa miaka 28 na kuendelea.
Waandishi wa Habari huchagua majina ya wachezaji 10 waliofanya vizuri katika mwaka na kuyapigia kura na huu ni mwaka wa kumi zikitolewa Tuzo hizo.

Andres Iniesta anakua mchezaji wa kwanza wa Barcelona na Spain kushinda tuzo hiyo alishindanishwa pia na  Cristiano Ronaldo, Nahodha wa England Wayne Rooney, Andrea Pirlo, Thiago Silva, Thiery Henry, Frank Ribery, Yaya Toure, Manuel Neuer na Marta.

 Iniesta aliambatana na mkewe Anna Ortiz katika tuzo hizo ambazo zimewahi kuchukuliwa na wachezaji nyota kama Ronaldinho, Zlatan Ibrahimovic,Ronaldinho, Ryan Giggs n.k

Katika Pozi Iniesta akiwa na Mkewe Anna
Mkali huyu wa Barcelona aliye na miaka 30 hivi sasa amekulia  Barcelona tangu mwaka 1996 alipost katika ukurasa wake wa Twita akiwashukuru wote waliompigia kura kushinda Tuzo hiyo. Na Jumanne hii anarudi Catalunya kwaajili ya mazoezi na klabu yake ya Barcelona ambayo inashindania kurudisha makali yake baada ya kupotea mwaka uliopita.

WASHINDI WA TUZO HIZO TANGU ZILIPOANZISHWA

  • 2003 - Roberto Baggio (Brescia)
  • 2004 - Pavel Nedved ( Juventus)
  • 2005 - Andriy Shevchenko (AC Milan)
  • 2006 - Ronaldo De Lima (Real Madrid)
  • 2007 - Allesandro Del Piero (Juventus)
  • 2008 - Roberto Carlos (Fanerbahce)
  • 2009 - Ronaldinho (AC Milan)
  • 2010 - Francesco Totti ( AS Roma)
  • 2011 - Ryan Giggs (Manchester United)
  • 2012 - Zlatan Ibrahimovich ( PSG)
  • 2013 - Didier Drogba ( Galatasaray)
  • 2014 - Andres Iniesta (Barcelona)

.... Imeandaliwa na Edo Daniel Chibo

++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++

1 comment:

Powered by Blogger.