HABARI 8 KALI ZA SOKA JANA JUMANNE
NYUMBANI
![]() |
Umati wa mashabiki katika moja ya pambano la watani |
1. Shirikisho la Soka nchini Tanzania TFF limewataka mashabiki kununua mapema tiketi za pambano la Watani wa jadi Simba na Yanga litakalopigwa Jumamosi hii.
Tiketi hizo ambazo zinauzwa kwa mtindo wa Eletroniki zimeanza kuuzwa juzi na zitauzwa mpaka siku ya mchezo kiingilio cha chini kikiwa ni 7,000 na cha juu ni 30,000.
2. Kipa wa Simba Ivo Mapunda amewasili katika kambi ya Klabu hiyo iliyoko jijini Johannesburg tayari kwa mazoezi ya mwisho kabla hawajaivaa Yanga Jumamosi hii.
Ivo aliachwa Dar es Salaam kutokana na maumivu lakini hivi sasa ameonekana yuko fiti.
ULAYA
3. Washambuliaji wa Barcelona Messi,Neymar na Suarez jana walidhihirisha kua wao ni balaa baada ya kufunga jumla ya magoli 8 wamiwa na timu zao za Taifa.
Neymar aliiongoza timu yake ya Taifa kuichapa Japan bao 4-0 huku yeye akifunga mabao yote. Suarez alifunga mabao mawili wakati timu yake ikicheza na Oman huku Messi naye akifunga mawili Argentina wakiifunga Hong kong 7-0.
4. Meneja wa Real Madrid Carlos Ancellot amesema Angel Di Maria amejiunga na Manchester United kwasababu ya pesa tu kwani alitaka pesa nyingi sana ili kubaki Madrid.
6. Manchester United wanaandaa mkataba mpya kwa kipa wake David De Gea wenye thamani ya paundi milioni 30 ili kumshawishi kipa huyo kuepukana na wazo la kutimkia Real Madrid wanaomtaka.
6. Javier Hernandez 'Chicharito' amesema anaamini kuwa hatorudi Manchester United pindi mkataba wake utakapoisha huku kocha Luis Van Gaal anatumai kiwango cha mshambuliaji kitakua ili aweze kuuzwa kwa bei nzuri. Chicharito yuko Real Madrid. Kwa mkopo akitokea Man United.
7. Adrian Mutu amezuiliwa kuchukua Visa yake ya kwenda nchini India baada kuonekana amelewa tilalila alipokua anafata Visa yake.
Adrian Mutu alitimula na Chelsea siku za nyuma baada ya kugundulika anatumia madawa yaliyokatazwa michezoni.
8. Kocha wa Chelsea Jose Mourinho amesema alikataa mara mbili kujiunga na Matajiri wa Ufaransa walipokua wanamhitaji aende akaifundishe timu hiyo.
... Kwa sasa ni haya tu tukutane tena badae leo kwa habari 8 kali za siku ya leo
.......Usisahau ku like ukurasa wetu Facebook (Wapenda Soka- kandanda)
{Edo Daniel Chibo}
No comments