MIAKA 18 YA ARSENE WENGER, MAFANIKIO NA MADHAIFU YALIYOWAGAWANYA MASHABIKI WA ARSENAL NA KOCHA WAO.
Leo hii tarehe 1 mwezi wa kumi Wenger ametimiza miaka 18, tangu amekuja Arsenal. Alitokea Japan, akiwa hajulikani kabisa. Hata watu wengi leo hii hawakutarijia kama angekaa mda mrefu kiasi icho. Ni mafanikio mazuri, kwa zama hizi za mpira wa kisasa, kocha kukaa miaka 18 kwenyi club moja.
Kwa kipindi hicho amekaa ameshinda mataji 3 ya ubingwa wa Uingereza, makombe 4 ya FA, 2006 alikua mshindi wa pili wa Uefa Champions league. Kilichompa umaarufu na heshima kubwa zaidi ni "invisible side" ya mwaka 2004. Baada ya msimu huo, wengi waliamini Wenger ametengeneza kikosi kitachotawala ulaya na uingereza kwa muda mrefu kidogo, lakini haikua hivyo.
Taratibu, miaka ilivyozidi kwenda nafasi ya kwanza ikawa nafasi ya nne, miaka ilivyozidi kwenda Arsenal ilipoteza umaarufu wake na kuanza kufungwa na timu ndogo kwenye "stage" kubwa au hatua nyeti kama Birmigham, Braga, Blackburn, na hata Bradford.
Haikuiishia hapo, vipigo vya aibu kwenye viwanja vya wapinzani wake kama 8-2 Old Trafford, 6-0 Stamford bridge, 5-1 Anfield, 6-3 Etihad, 4-0 Sansiro navyo vimekua vikitokea siku za karibuni. Hii inaashiria ni upotevu wa fikra ya kiushandani dhidi ya wapinzani, ambayo ilianza taratibu kama ugonjwa wa kansa.
Waandishi, mashabiki wa mpira/arsenal na wachambuzi wa soka kila mtu ana maoni yake, ni sababu gani imesababisha kuanguka kwa Arsenal kwa kipindi hicho cha miaka 10. Wengine wanasema ni sababu ya kuondoka kwa David Dein (aliyemsaidia sana Wenger kwenye usajili na "scouting" pia), wengine wanasema ni ujio wa wawekezaji kama Roman Ambromovich, wengine wanasema ni kufanya mpira kwa njia sahihi zisizo na shortcut ( kinyume na kina Sheikh Mansour na Abromovich).
Maswali ni mengi lakini majibu yanaweza yakawa mengi, au machache, au yasiyo ya kuridhisha. Mimi binafsi kama shabiki wa mpira na shabiki wa Arsenal, naamini Arsene Wenger angetakiwa kwa namna moja au nyingine kupata mafanikio zaidi ya aliyopata sasa, ndani ya miaka kumi iliyopita (2004-2014) bila kuangalia hali ya Arsenal, au wapinzani wake wamefanyaje, alitakiwa kufanya vizuri zaidi.
Mashabiki wa arsenal kwa sasa, inapofika swala la Wenger wamegawanyika pande mbili. Wako wanaosema, "Wenger aondoke, hafai kwa zama hizi, muda wake umeisha" Wapo wengine wanasema "Hapana, Wenger abaki, ndio mtu sahihi wa kuirudisha Arsenal mahala pake".
Lakini ukiuliza hawa ambao wanapenda Wenger abaki, sababu zao ni zipi, majibu yao kidogo yanazidi kupitwa na wakati kwa sababu miaka inakwenda, na ushindani unaongezeka, sio kwamba naungana nao, au nawapinga lakini najaribu kuangalia mtazamo wao..
Majibu yao ni kama yafuatayo:
1. Mpeni mda wa kutosha, mambo yatakaa sawa.
2. Amekua hapewi hela ya kutosha, hawezi kushindana na mabilionea wa PSG, Man City, Chelsea n.k
3.Ngoja FFP ikianza utaona faida za Wenger
4. Hakuna kocha anaweza kutuweka nafasi ya 4 miaka 18 zaidi ya Wenger.
5. Angalia tusije kua kama Liverpool au Man United ya Moyes.
6. Anatengeneza timu, ngoja Wilshere, Ramsey, Ozil wakue na wazoeane.
Sababu ya 1,2, na ya 3 ni ya kweli kabisa na yalikua active mpaka 2010/2011. Lakini sio mpaka saivi.

Budget ya Mshahara wa Arsenal sasa hivi inakaribiana au inatofautiana kidogo sana na Chelsea. Kwa hiyo Arsenal kiuchumi imeanza kua imara tena. Sababu za nne na za kuendelea, mimi naziita "non-sense" (siyo za msingi)
Arsenal ndiyo timu inayoongoza kwa tiketi ghali zaidi kwenye uwanja wake, ulaya nzima, na mwaka huu baada ya deni kuisha, mashabiki walitegemea, tiketi zitashuka, kinyume chake, bei ya tiketi imeongezeka kwa 3%. Mimi sijui kwa nini, lakini naamini bodi inayo sababu maalum kwa hilo.
Kitu kibaya kinachotia wasiwasi ni uwezo wa Arsenal kucheza na timu kubwa, umekua ukipungua miaka inavyozidi kwenda. Kwa miaka kadhaa sasa Arsenal inashindwa kushinda mechi zenye "pressure" kubwa. Hili tatizo ni la kisaikolojia, wala si la kiuwezo na muhusika wa kutatua tatizo ili ni mzee Wenger. Baadhi ya makocha sasa wanajua ni kitu gani wakisubirie wakicheza na arsenal, kwa iyo wanaandaa mfumo mzuri tu wakujizatiti, na wanafanikiwa, ili liko wazi. Hakuna shabiki wa Arsenal anajiamini wakicheza na Chelsea, Man City, Man Utd achilia mbali vilab vikubwa kama Bayern Munich, R.madrid na Barcelona. Hili ni tatizo la linaelekea kua ugonjwa sungu kwa kadri muda unavyozidi kwenda.
Kitu kingine ambacho nacho kinamuhusu Wenger kwa 100% ni usajili. Arsenal haiwezi kushindana na Chelsea, Man City n.k sawa lakini kuna baadhi ya wachezaji arsenal kuwapata hawaitaji kuvunja benki kuwapata.
Mwaka 2005/2006 Arsenal ilikua na shida ya golikipa, Edwin van de sar, alikua anapatikana kwa bei rahisi tu na wenger alipewa pendekezo ili amchukue. Lakini alienda kumnunua Emanuel Almunia, Mark shwazer alikua anapatikana kwa paundi 3 tu mwaka 2009, na bado Arsenal ilikua na tatizo la kipa lakini, mzee alifumba macho.
Wenger huyu huyu ndiye aliyelipa 6 million kwa Andre Santos , 11milion kwa Gervinho, 5milion kwa Squillaci na kituko kikubwa zaidi ni kutoa 5 kwa kumnunua Park kutoka monaco. Kwa bei izo izo kama Wenger angefanya "scouting" ya maana angepata wachezaji wazuri tu wenye hadhi ya Arsenal. Kwa kuwa alifanya kwa Ljungberg, Pires, Wiltord basi alijua kuwa na hiyo itamlipa, bila kuangalia alama za nyakati.
January 2014, Arsenal ilikua na shida kubwa ya mshambuliaji, na ilikua inaongoza ligi. Na ilionekana wazi Olivier Giroud ameelemewa ili kuendelea kuongoza ligi, kila mtu aliona arsenal iliihitaji wachezaji wawili au hata mmoja mzuri lakini. Matokeo yake Wenger alienda kununua mchezaji majeruhi (akiwa anafahamu ni majeruhi) Kim Kallstrom. Na alicheza mechi 4 tu kwa miezi 5.
Msimu uliopita Arsenal iliongoza ligi kwa siku 128, Chelsea iliongoza ligi kwa siku 63, Liverpool siku 54, na mabingwa Man City siku 15. Kwa iyo unapata picha gani? Arsene Wenger angejua udhaifu wa timu yake, angesajili na hatimaye, nani anaejua labda angetwaa ligi. Kukaa pale kwa siku 128 sio kwamba unabahatisha, timu yako iko vizuri, kwanini hakulifikiria hilo januari? Na ndiyo ilikuwa nafasi pekee.
Msimu ukiisha, kocha inabidi usome matatizo ya msimu ulioisha na ufanyie kazi kwa ajili ya msimu unaokuja.
Chelsea iliona ina shida ya kiungo mchezeshaji na mshambuliaji. Wakaenda mnunua Fabregas na Diego Costa kwa bei za kawaida tu na tatizo likatatuliwa.
Arsenal kwa macho ya kawaida ilionekana kuna shida ya beki wa kati, baada ya kumuuza Vermalean, kiungo mkabaji (especially baada ya vipigo vizito) winga mfungaji na msaidizi wa Olivier Giroud.
Sanches sawa kabisa. Welbeck sawa tu japokua si mzuri sana. Vipi kuhusu beki wa kati na kiungo mkabaji? Vipi hauoni Arteta umri unaenda, majeruhi yanamuaribia, na Flamini ayo majukumu hayawezi??
Je hauoni kuwa Koscienly na Mertesecker wanahitaji msaada?? Wataweza cheza mechi ya 50 baada ya World cup? Je chambers ni kijana wa kutegemea azibe mapengo yote ayo akiwa na miaka 19??
Naamini kwa miaka hiyo yote iliyopita bila makombe, Arsenal na Arsene wenger bado wangeweza kufanya kitu. Baada ya kuchukua ubingwa 2004, Wenger bado angeweza kujenga timu ya kiushandani bila ya hata ya kua na hela nyingi kwa kua, uzoefu anao, na mtizamo wa ushindi ulikuepo.
Na kama huwezi kushindana na hao "big boys" yupo mtu wa pili mwenye hisa nyingi hapo arsenal ambaye ana hela nyingi kuliko mtu yoyote uingereza, ambae pia ni shabiki mkubwa wa Arsenal, Mr Ulishar Usmanov. Lakini bodi ya arsenal ilimnyima kununua share nyingi arsenal na kumpa nafasi "Mr silent man" Stan kroenke. Sababu kwa kweli sizifahamu za hicho kitendo, lakini ni jambo la kutia wasiwasi.
Kwa miaka 18 ya Wenger kuwa na Arsenal, nafikiri kuna baadhi ya maamuzi ambayo ameyafanya, na yalisababisha kwa namna moja au nyingine Arsenal kutokuwa na mafanikio zaidi. Kama aliweza shinda ligi hii mara 3, na kama aliweza ongoza ligi kwa siku 128, basi uwezo anao, ni jeuri, kiburi, na falsafa zake ndizo zinazomwangusha.
Ni kikosi na saikolojia tu, mfano mzuri ni Athletico Madrid, hawana hela za kushindana na Real Madrid au Barcelona lakini bado ameweza pambana nao, kwa kutumia akili na nguvu kazi aliyonayo.
Asanteni
Frank Victor (member: Wapenda Soka)
0717 722 141

Hili bandiko ni hatari sana umenifanya nikumbuke bandiko jingine lilitolewa hapa hapa likisema Wenger na sera za azimio la Arusha. Bandiko hilo liko hapa kwenye link
ReplyDeletehttp://wapendasoka.blogspot.com/2014/09/wenger-na-azimio-la-arusha.html
Aisee frank big up sana
ReplyDelete