LIGI YA MABINGWA ULAYA LEO : RONALDO KATIKA MBIO NDEFU KUMPITA RAUL NA MESSI



Ligi ya Mabingwa Ulaya inaendelea tena usiku wa leo katika mechi za awamu ya pili katika makundi ambapo miamba 16 itajitupa uwanjani katika viwanja 8 kujaribu kupata pointi za kuzivusha hatua hii.

Arsenal baada ya kufungwa 2-0 na Dortmund katika mechi ya awali leo watakua katika dimba lao la nyumbani kuwakaribisha Galatasaray toka Uturuki ambao walitoka sare na Anderletch katika mechi ya awali.

Mabingwa wa Spain Atletico Madrid wao watakua nyumbani Vicente Calderon kuwakaribisha mabingwa wa Italia klabu ya Juventus maarufu kama kibibi kizee cha Turin.
Atletico Madrid wanaingia katika mchezo wa leo wakiwa na kumbukumbu ya kupoteza mchezo wa awali dhidi ya Olympiacos wakifungwa ugenini 3-2. Wakati Juventus wao watakua na kumbukumbu nzuri ya ushindi wa bao 2-0 dhidi ya Malmo FC.



Mabingwa watetezi Real Madrid wako Bulgaria kucheza na klabu ya Ludogorets huku macho na masikio yakiwa kwa mchezaji bora wa dunia Cristiano Ronaldo ambaye yeye na Messi wanawania kuvunja rekodi iliyowekwa na Raul ya kufunga mabao mengi katika michuano hiyo wakiwa wameshafunga Magoli 68 kila mmoja wanawania kupita rekodi ya Raul Gonzalez ambaye amedumu muda mrefu na rekodi yake ya mabao 71.
Ronaldo akiwa katika mbio ndefu hivi sasa kwa kupachika mabao baada ya kufunga magoli 7 katika mechi 2 anaonekana anaweza kuvunja rekodi leo.
Nini kitajiri endelea kutembelea ukurasa huu kwa habari za uhakika.

RATIBA KAMILI YA MECHI ZA LEO

GROUP A
21:45.  Malmo vs Olympiakos
21:45.  Atletico Madrid vs Juventus

GROUP B
21:45. Ludogorets vs Real Madrid
21:45. FC Basel vs Liverpool

GROUP C
19:00.  Zenit vs Monaco
21:45.  Bayer Levrekusen vs Benfica


GROUP D
21:45.  Anderletch vs Dortmund
21:45. Arsenal vs Galatasaray

NOTE: MUDA NI KWA SAA ZA AFRIKA MASHARIKI.

No comments

Powered by Blogger.