HESABU ZA INJINIA PELLEGRIN NA MAAFA YA MAN CITY

Manuel Pelegrini


 Maisha yanaenda kasi sana na mazoea yana tupotezea  muda  haswa wajenzi. Wao daima wako bize na kazi yao ya ujenzi ila tofauti na wajenzi wengine mjenzi huyu Manuel Pellegrin yeye hana muda wa kukokotoa mahesabu kwa ajili ya ujenzi wa kila jengo analojenga.

Yes! Manuel Pellegrin kocha mkuu wa mabingwa watetezi wa ligi kuu England Manchester City ambaye ni mjenzi wa Manchester City huyu jamaa ameonekana yuko tofauti na wajenzi wengine na hapa ndo nakumbuka maneno ya Kelvin Kilbane ambaye ni  mchezaji wa zamani wa Everton ambaye amenukuliwa akisema "Man City are under pressure"

Unaweza kukataa kwakua unawaona wanacheza vizuri wanapokutana na Everton  na wana mfunga kiurahisi Man United. Tatizo la Man City ni huyu mjenzi wao raia wa Chile Manuel Pellegrin ambaye anaamini presha ya Everton ni sawa kabisa na ile ya As Roma au ile ya Bayern Munich. Hapa naona mjenzi huyu anaanza kushindwa kwani Namwona mjenzi huyu anajaribu kuwaaminisha Man City kwamba jumba analojenga la gorofa 100 ( ligi ya mabingwa Ulaya) wanaweza kupanda kwa kutumia ngazi na wakafika sawa na yule anayetumia lifti hivyo hawahitaji lifti.



Kwa umakini mkubwa nimerudia mechi kadhaa alizocheza Totenham Hotspurs akiwa mashindano ya Ulaya nimegundua kua unahitaji fundi ujenzi na injinia mwenye uwezo wakucheza na vifaa vyake vizuri bila kujali thamani yake.
Usiku wa jana injinia huyu alikuja eneo la ujenzi bila pima maji  ya Fernando na Mangala ambao wao wameletwa kufanya hiyo na kwa usiku wa Jana walihitajika sana kulipima jengo la  Rudi Garcia ambaye ni mjenzi wa jengo la pili kwa urefu katika Serie A pale Italia. Naizungumzia AS Roma toka Italia.

Hapa ndo unaweza ukajiuliza maswali kama Je Gael Clichy alikua anashindwaje kumlinda Gervinho wa As Roma? Achana na Gervinho mwiba ulikua ni  mkongwe Francesco Totti ambaye mimi nasema uzoefu wake hauna mbadala hebu cheki alivyo chukua mpira kwa ustadi mkubwa katika umri wa miaka 38 huku akifunga magoli hatari ukikaa vibaya jengo lote analishusha chini bila kujali nani alikua Injinia.

 Ingawa Man City hawakua wabaya sana kwa mechi ya jana hasa baada ya kamanda Yaya kuamka toka usingizini kipindi cha pili lakini mimi nadhani udhaifu ulitokana na mtindo wa Injinia Pellegrin  kuamini kua ni Yayaa pekee ndiyr anayeweza Ibeba Man City.
 Sasa jiulize umeshawahi kusikia David Silva analaumiwa timu ikifungwa? Nadhani kimoyomoyo unasema HAPANA na hapa ndipo utaamini kuwa Injinia Pellegrin anajaribu kutuaminisha kua Man City ni Yaya na Yaya ni Man City.
Man City wanakosa kutumia usemi usemao "kila kona bao" nadhani huu ndio mtindo ninaao uona upo katika ligi ya Mabingwa kwani hatuhesabu ni jinsi gani ulicheza vizuri bali pointi tatu za kukuvusha na hapa ndipo Man City wanapo shindwa na wamekua wageni na niwageni haswa.

Injinia Pellegrin  itambidi ajiulize kwa umakini mkubwa je aendelee kucheza mashindano au akubali tu kufurahisha watu na hapa nikiwa namaana kua nikweli AS Roma wenye pointi 4 na Bayern Munich wenye pointi 6 wataachia nafasi ili Man City apite au tutumie usemi ule wa kua huu ni mpira bwana lolote linaweza tokea?
Au ampigie simu Wenger kumuuliza anatimia mzizi gani ili naye atumie.

By lucas_tz ( member: Wapenda Soka)
0764665151
×××××××××××××××××××××××××××××××××××××××××××××××××××××××

No comments

Powered by Blogger.