MAN UNITED KATIKA MIAKA 10 YA KUHARIBU REKODI YA ARSENAL NA KUJARIBU KUIVUNJA REKODI YACHELSEA
Leo imetimia miaka 10 kamili tangu Manchester United ilipovunja mwiko wa kuifunga Arsenal ambayo ilishinda ubingwa wa Ligi Kuu Nchini England bila kufungwa.
Hii ndiyo Arsenal bora kabisa na ndo timu bora kuwahi kutokea Tangu ligi kuu England ilipoanza upya mwaka 1992.
Ikicheza katika mchezo wake wa 49 bila kufungwa ilitembelea uwanja wa Old Trafford ambapo ndo ilipokua mwisho wa kucheza msimu mzima katika ligi bila kufungwa kwani siku hiyo Oktoba 24 mwaka 2004 ambapo Man united iliibuka na ushindi wa bao 2-0.
Magoli ya Man united Siku hiyo yalifungwa na Ruud Van Nisterlrooy kwa penati baada ya Wayne Rooney kuangushwa katika eneo la hatari na Sol Campbell wa Arsenal.
Bao la pili la United lilifungwa na Wayne Rooney baada ya kupokea pasi ya Alan Smith toka upande wa kulia wa uwanja.
Man United Jumapili hii watakua tena Old Trafford kujaribu kuwazuia Chelsea ambao wameanza msimu huu bila kufungwa wakiwa wanaongoza Ligi wakiwa nafasi ya kwanza na pointi zao 22 huku United wakishika nafasi ya 6 wakiwa na pointi 12 ikiwa ni tofauti ya pointi 10 baina yao. Swali litakua je Man united wataendeleza ubabe kwa hizi timu ambazo hufika Old Trafford wakiwa na Imani ya kupata pointi mwishowe huisha kupoteza na kuharibiwa rekodi yao.
MLINGANISHO
- Katika mechi 5 zilizopita Man United imeshinda mechi 3 na kutoa sare mechi moja huku ikipoteza mechi moja wakati Chelsea wao katika mechi 5 zilizopita wameshinda mechi zote na kuifanya kuwa timu inayoogopwa sana na kupewa nafasi kubwa kuchukua ubingwa msimu huu.
- Katika mechi 5 zilizopita baina ya timu hizo Chelsea imeshinda mechi 3 huku mechi mbili zikiisha kwa sare na United haijawahi kuifunga Chelsea katika mechi hizo 5 zilizopita.
- Mechi ya mwisho baina ya timu hizo ilishuhudiwa United ikiambulia kichapo cha bao 3-1 magoli yote ya Chelsea yakifungwa na Samuel Eto huku mechi ya mwisho kupigwa katika dimba la Old Trafford Timu hizo zilitoka sare ya bila bila ikiwa ni Tarehe 26 Agosti mwaka Jana.
HALI ZA TIMU
Chelsea pengine inaweza kumkosa washambuliaji wake Diego Costa na Loic Remy ambao ni wagonjwa.
Angel Di Maria anaweza kuanza katika mchezo huo kwa upande wa United katika mechi ambayo Man united itamkosa tena Nahodha wake Wayne Rooney ambaye anatumikia adhabu ya kufungiwa michezo mitatu na huo mchezo dhidi ya Chelsea ndo utakua wa mwisho kwake akiwa "kifungoni"
Ni mechi itakayowakutanisha Mwalimu ( Van Gaal) na mwanafunzi wake (Mourinho) ambao walikua pamoja Barcelona wakati Van Gaal akiwa ndo kocha na Mourinho mmoja wa wasaidizi wake.
Chelsea ikiwa imekamilika zaidi idara ya kiungo United wao wamekamilika katika ushambuliaji.
Van Gaal atakua anaingia na mbinu moja tu ya kuwazuia Chelsea wasimshambulie sana kwa kuwawekea washambuliaji watakaoiogopesha Chelsea kwenda kushambulia ovyo.
Mechi hii Itaanza saa 1 kamili jioni na mwamuzi atakua Phil Dowd mwamuzi ambaye Kocha wa Zamani Wa United Sir Alex Ferguson aliwahi kumtuhumu kua alinenepa na hawezi kwenda na kasi ya mpira.
TUKUTANE JUMAPILI
~ Edo DC
No comments