LIGI YA MABINGWA ULAYA : RONALDO ABAKIZA GOLI MOJA KUMFIKIA RAUL



Jumla ya magoli 19 tu yalifungwa katika hatua ya tatu ya michezo ya makundi katika ligi ya Mabingwa Barani Ulaya usiku wa jana  ikiwa ni tofauti na magoli 40 yaliyofungwa siku ya Jumanne. Magoli ambayo yalivunja rekodi katika magoli mengi yaliyofungwa kwa usiku mmoja.

Mabingwa watetezi Real Madrid wakiwa Ugenini katika uwanja wa Anfield jijini Liverpool waliweza kuibuka na ushindi wa bao 3-0 ukiwa ni ushindi wa 3 mfululizo tangu kuanza kwa msimu mpya wa Ligi ya Mabingwa.



Cristiano Ronaldo alifunga goli lake la 70 katika historia ya michuano hiyo ambapo amebakisha goli moja tu kuifikia rekodi ya Raul Gonzalez ambaye ameshawahi kufunga magoli 71 katika michuano hiyo akiweka rekodi ambayo haijavunjwa mpaka sasa japokua Ronaldo na Messi wanaikaribia kuivunja.

Katika listi ya wachezaji waliofunga mabao mengi katika ligi ya mabingwa barani Ulaya Raul anashika usukani akiwa na magoli 71, anafatiwa na Ronaldo mwenye magoli 70, Messi anashika nafasi ya 3 akiwa na magoli 69, Ruud Van Nisterlooy anakamata nafasi ya 4 akiwa amefunga magoli 56 huku Thierry Henry anakamata namba 5 na magoli 50 aliyowahi kuyafunga akiwa na Arsenal.

Magoli mengine mawili yalifungwa na Karim Benzema ambaye yeye Ronaldo na Isco waliisumbua mno ngome ya Liverpool. Wakimtumia Balotel kama mchezaji pekee pale mbele Liverpool walionekana kuzidiwa kimchezo mpaka mapumziko lakini baada ya Mapumziko aliingia Adam Lallana ambaye alirudisha uhai kwa timu hiyo.

Mchezo mwingine uliishuhudia Arsenal ikipata magoli mawili ya haraka dhidi ya Anderletch katika mchezo ambao iliwabidi vijana wa Arsene Wenger kusawazisha na kupata ushindi katika dakika za lala salama.

MATOKEO KAMILI NA WAFUNGAJI KATIKA MICHEZO YA JANA

● Atletico Madrid 5-0 Malmo FF

Koke (48')
Mandzukic (61')
Griezmann (63')
Godin (87')
Cerci (90')

● Olympiakos 1-0 Juventus

Pajtim Kasami (35')

Liverpool 0-3 Real Madrid
Cristiano Ronaldo (23')
Karim Benzema (30')
Karim Benzema (41')

● Ludogorets Razgrad 1-0 FC Basel

Minev (90')

● AS Monaco 0-0 Benfica


Bayer Leverkusen 2-0 Zenit St Petersburg

Donati (58')
Papadopoulos (63')

● Anderlecht 1-2 Arsenal

Najar (72')
Gibbs (89')
Podolski (90')

● Galatasaray 0-4 Borussia Dortmund

Pierre-Emerick Aubameyang (6')
Pierre-Emerick Aubameyang (18')
Marco Reus (41')
Ramos (83')

×××××××××××××××××××××××××××××××××××××××××××××××××××××××

No comments

Powered by Blogger.