EL CLASICO : RONALDO ANATAFUTA REKODI HAT TRICK NYINGI, MESSI MAGOLI MENGI ZAIDI LA LIGA
Mechi ya watani wa jadi Tanzania yani Yanga na Simba iliyopigwa katika dimba la Taifa wiki iliyopita ilikua ni kati ya mechi zilizovuta hisia kubwa kwa mashabiki wa soka Tanzania ndo mechi ambayo inazungumziwa sana katika Tanzania.
Hii sio kwa Tanzania tu kuna nchi nyingi zinatokea mechi ambazo huwa na ushindani huu na hubeba historia kama watani wa jadi.
Kenya wana Gormahia na AFC Leopards, Italia wana Inter Milan na AC Milan, kule Argentina kuna Boca Juniors na River Plate n.k
Achana na hizo njoo katika El Clasico hii ni mechi inayowahusisha wapinzani wa jadi katika soka la Spain yani Real Madrid na Barcelona ni mechi ambayo inakadiriwa kuwa itatazamwa na watu milioni 500.
Huwezi shangaa ukawaona Richard Leonce na Van Tall toka Wapenda Soka Tanzania wakibishana utadhani wanaishi Spain. Kila kona ya dunia tunaizungumzia mechi hii na leo Kwa mara nyingine ulimwengu wa Soka unashuhudia pambano hilo likiwa ni labkwanza kwa msimu huu kati ya wakali hao wa Spain.
Historia inasema mwaka 1943 Barcelona walishawahi kufungwa bao 11-1 katika mechi ya El Clasico wakiwania kombe la mfalme (Copa Del Rey) sitegemei hii kujirudia katika pambano la leo kwani nafasi ya kumwacha mtani wako akafunga magoli yote hayo siioni ikitokea katika vikosi ambavyo vina wakali wa kupachika mabao kama Lionel Messi, Neymar na Suarez kwa upande wa Barca huku Madrid wakiwa na Ronaldo,Bale na Benzema (BBC) hapo sitegemei hata pambano kuisha kwa 0-0 lazima utashangilia goli.
HISTORIA
- Hii ni mechi ya 229 kati ya wapinzani hao katika mashindano yote tangu zilipoanzishwa hizi timu. Huku Real Madrid wakishika rekodi ya kuwa wababe wakiongoza kwa kushinda mechi 91 huku Barcelona wakishinda mechi 89 na mechi 48 zikiisha kwa sare.
- Lakini licha ya Real Madrid kuwa wababe, Barcelona wamekua wanainyanyasa mno Real Madrid katika miaka ya hivi karibuni kwani katika mechi 12 zilizopita,Barcelona wameshinda 8 kati ya hizo ikiwa na ushindi wa nyumbani na ugenini msimu uliopita.
- Ukiacha yale magoli 11-1 waliyofungwa Barcelona mwaka 1943, Ushindi wa bao 5-0 walioupata wakali hao wa Catalunya mwaka 2010 ilikua ni ushindi uliotawaliwa na kiwango bora kabisa kwa Barcelona.
KINACHOTARAJIWA
Macho ya wengi leo yatakua si kwa Lionel Messi na Cristiano Ronaldo pekee bali pia kwa Luis Suarez ambaye jana alikamilisha kifungo cha miezi minne na leo anaweza kuanza katika safu ya ushambuliaji ya Barcelona ambayo imeonekana kua butu licha ya kuongoza katika ligi mpaka sasa.Lionel Messi anahitaji goli moja tu kufikia rekodi ya kuwa mchezaji aliyefunga magoli mengi katika ligi kwani Messi ana magoli 250 anahitaji hilo goli moja kumfikia Telmo Zarra aliyekua mchezaji wa Atletico Bilbao miaka ya 1940 ambaye aliweka rekodi ya kufunga magoli 251.
Real Madrid wasingependa kumwona Messi anavunja rekodi katika uwanja wao na ikizingatiwa Rais wa La Liga Javier Tebas aliyenukuliwa anasema kama Messi atafunga magoli mawili au zaidi na kuweka rekodi mpya uwanja utasimama kumpa heshima.
Mbele ya Ronaldo ambaye ni mchezaji bora wa Dunia Real Madrid watafanya kila liwezekanalo kushinda mechi hiyo na kumzuia Messi kuvunja rekodi.
Cristiano Ronaldo ataingia katika mchezo wa leo akiwa ameshafunga magoli 15 katika michezo 8 ya Ligi akiweka rekodi ya mchezaji aliyefunga magoli mengi katika mechi 8 za ufunguzi katika ligi.
Jumla ya magoli 15 ambayo Ronaldo ameshayafunga msimu huu anakua ameshafunga magoli mengi katika ligi kuzizidi zaidi ya timu 81 kati ya timu 98 katika ligi 5 kubwa barani Ulaya wakiwemo pia Mabingwa watetezi wa La Liga Atletico Madrid, Liverpool na Arsenal ambao hawajafikia magoli 15 msimu huu.
Ronaldo na Messi leo wanatafuta kuvunja rekodi tofauti tofauti. Ronaldo kama atafunga magoli matatu au zaidi leo atakua amevunja rekodi ya mchezaji aliyefunga magoli matatu au zaidi (hat trick) mara nyingi kuliko mchezaji yoyote katika historia ya La Liga kwani mpaka sasa ameshafunga magoli ya namna hiyo mara 22 sawa na Alfred di Stefano na. Telmo Zarra.
Wakati Messi yeye anatafuta rekodi ya kuwa mchezaji aliyefunga magoli mengi zaidi katika historia ya La Liga iwapo atafunga magoli mawili au zaidi.
Ukiacha uwanja wa Nou Camp nyumbani kwa Barcelona, Uwanja wa Real madrid Santiago Bernabeu unafatia kwa kuweza kuingiza watu wengi zaidi una uwezo wa kuingiza watazamaji 81,044 na hao wote wanatarajia kuhudhuria katika pambano hilo.
Mechi hii inatarajia kuanza saa 1 usiku kwa saa za Afrika Mashariki hupaswi kukosa hii mechi kama Mpenda Soka.
Asanteni
Prepared by : Edo Daniel Chibo
Email : wapendasoka@gmail.com
Mobile: + 255 715 127272
Page: facebook.com/wapendasoka-kandanda
No comments