HABARI 8 KALI ZA SOKA MCHANA HUU


        NYUMBANI

1. Klabu ya Simba imesafiri kuelekea nchini Afrika Kusini kujiandaa na mechi dhidi ya Yanga itakayopigwa Jumamosi ya wiki ijayo tarehe 18 katika dimba la Taifa Jijini Dar Es Salaam

2. Beki wa Simba Joram Mgeveke ameongezwa katika kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania kujiandaa na mchezo wa kirafiki dhidi ya Benin. Joram anaungana na beki toka Azam Gardiel Michael na kiungo Jonas Mkude wa Simba.



3. Kenya ni kati ya Timu 7 zilizopita katika mchujo wa mwisho wa kuwania nafasi ya kuandaa kombe fainali za kombe la mataifa ya Afrika. Ombi la Tanzania limepigwa chini kutokana na kutotimiza vigezo vya kuandaa kwanza fainali za vijana.
Nchi nyingine zinazowania kuwania nafasi ya kuandaa fainali hizo zitakazofanyika mwaka 2017 ni Misri,Algeria,Ghana,Zimbabwe,Sudan na Gabon.

4. Kiingilio cha chini katika mechi ya Kirafiki ya Kimataifa kati ya Tanzania na Benin ni shilingi 4,000 kwa mashabiki wa jukwaa la Bluu na na kijani. VIP B itakua ni 10,000. VIP C na A viti vyake vimetengwa kwa wageni maalumu.

ULAYA


5. Barcelona watatimuliwa kushiriki La Liga kama mpango wa kujitenga kwa jimbo la Catalunya utafanikiwa. Jimbo la Catalunya kwa muda mrefu limekua likipigania kujitenga na kuwa nchi huru na mwezi ujao itapigwa kura ya maoni kuhusu jambo hilo. Barcelona na Espanyol zinatoka katika jimbo hilo. Ulishawahi kufikiri ligi ya Spain itakuaje kama Barcelona hawatakuwepo?

6. Beki wa Arsenal na timu ya taifa ya England Calum Chambers anaweza kuanza katika mechi ya kesho wakati England itakapopambana na San Marino katika mfululizo wa mechi za kuwania kufuzu kombe la mataifa ya Ulaya. Chambers anaweza kuanza kama Beki wa kati akishirikiana na Garry Cahill. Aliitwa kikosini baada ya kuumia kwa John Stones.

7. Kipa Wa Chelsea Petr Cech anafikiria kuihama klabu hiyo kufuatia kukosa namba kwasasa baada ya kocha Jose Mourinho kumtumia Thibaut Courtois katika mechi nyingi hivi sasa na Cech anafikiri ni muda muafaka sasa wa kutafuta changamoto mpya sehemu nyingine.

8. Roy Keane amesema katika kitabu chake kipya kuwa Sir Alex Ferguson alimlazimisha kuvaa jezi namba 7 ambayo ni maarufu sana na yenye historia kubwa kwa klabu ili kumzuia David Bechkam asiivae jezi hiyo. Keane anasema baada ya kuondoka Cantona mwaka 1997 Ferg alimwita na kumtaka kuchukua jezi hiyo lakini alikataa.


...Zimeandaliwa na Edo Daniel Chibo
{ 0715 12 7272 - whatsapp }
{ wapenda soka - kandanda : facebook}

No comments

Powered by Blogger.